Home LOCAL WATUMISHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

WATUMISHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI


Na.Alex Sonna_DODOMA

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Bw. Hamza Johari, amewataka watumishi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufanya kazi kwa weledi ili kuongeza ubora na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siki ya kuwatumikia wananchi.

Bw. Johari amesema hayo jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji, Dk. Eliezer Feleshi iliyofanyika mji wa kiserikali Mtumba.

Alisema, watumishi wa ofisi yake wanapaswa kufanya kazi kwa weledi ili kuongeza ubora na ufanisi katika kuwahudumia wananchi wenye changamoto mbalimbali za kisheria.

“Niwaombe watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria mkuu kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili kuongeza ubora na ufanisi wakati wa kutekeleza majukumu yenu ya kuwahudumia Watanzania”alisema
Kwa upande wake, Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi amewasisitizia Menejimenti na Watumishi wa Ofisi hiyo kutoa ushirikiano kwa Mwanasheria Mkuu na Naibu Mwanasheria Mkuu wakati wote ili kuongeza ufanisi.

Previous articleMAVUNDE AZITAKA BENKI KUIUNGA MKONO BENKI YA CRDB KUWAKOPESHA WACHIMBA MADINI
Next articleRAIS SAMIA AWAKONGA MOYO SINGIDA MASHARIKI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here