Home LOCAL TALGWU YAIPONGEZA SERIKALI KUWALIPA MSHARA WATUMISHI WA HALMASHAURI KUPITIA HAZINA

TALGWU YAIPONGEZA SERIKALI KUWALIPA MSHARA WATUMISHI WA HALMASHAURI KUPITIA HAZINA

Katibu Mkuu wa Chama  cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Bw. Rashid Mtima, akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Chama hicho leo Agosti 14,2024, Jijini Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU, kimeipongeza Serikali kwa kuwahamisha watumishi waliokuwa wanalipwa mishahara yao kwa mapato ya ndani ya Halmashauri (GF) ambapo sasa wanalipwa kupitia Mfuko Mkuu wa Serikali (HAZINA).

Amesema kuwa kuanzia mwezi Julai mwaka huu, Serikali imeshaanza kuwalipa wanachama 465 kati 645, na kwamba hatua hiyo ni kubwa kwani itaondoa kero za muda mrefu na kuongeza nguvu na morali ya kufanyakazi kwa ufanisi.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 14,2024 katika Ofisi za TALGWU, Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama hicho Bw. Rashid Mtima amebainisha kuwa kilio hicho cha kuhamishwa kwa watumishi hao kilikuwa cha muda mrefu na kwamba hatua hiyo inapaswa kupongezwa.

Aidha, ameeleza kuwa pamoja na pongezi hizo wanaiomba tena, Serikali kuangalia upya na kufanya mchakato ili wanachama wengine 180 waliosalia katika majiji na manispaa ambao bado wanaendelea kulipwa mishahara yao kupitia mapato ya Halmashauri, nao waanze kulipwa kupitia HAZINA.

”Kigezo kinachotumika kwamba Halmashauri walizopo zina makusanyo makubwa ya fedha zinazotokana na mapato ya ndani, na kwamba ziendelee kuwalipa mshahara wanachama hawa, tunaona ni wazo jema lakini bado si suluhisho la kutatua kero ambazo wamekuwa wakizipata hapo awali,” alisema Mtima.

Ameongeza kwa kuwataka Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo bado watumishi wanalipwa mshahara kupitia mapato ya ndani, kuhakikisha wanawalipa kwa wakati kama ambavyo inafanya HAZINA.

Amebainisha kuwa endapo Halmashauri hizo zitalipa mishahara ya watumishi hao kwa wakati ,itaondoa ombwe kubwa lililopo katika upatikanaji wa haki na stahiki za wanachama 180 waliosalia, na kuondoa matabaka ya kiutumisi mahali pa kazi.

Amezitajia Halmashauri ambazo bado zinalipa kwa kupitia mapato ya ndani kuwa ni Geita Mji, Ilala Jiji, Manispaa ya Kinondoni, Mbeya Jiji, Jiji la Mwanza, Temeke Manispaa, Dodoma Jiji na Manispaa ya Morogoro.

mwisho.

Previous articleTMX TUMEANZA MAANDALIZI MSIMU WA KOROSHO 2024/2025
Next articleRC CHALAMILA ATAKA WAKAZI WA JIMBO LA UBUNGO KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here