Home BUSINESS NAIBU WAZIRI NYONGO ARIDHISHWA NA TIC INAVYOVUTIA WAWEKEZAJI NCHINI

NAIBU WAZIRI NYONGO ARIDHISHWA NA TIC INAVYOVUTIA WAWEKEZAJI NCHINI

DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Mipango na Uwekezaji Stanslaus Nyongo, ameeleza kuridhishwa na hatua kadhaa ambazo zimeendelea kuchukuliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), katika kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa ajili ya Kuwavutia Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Naibu Waziri Stanslaus Nyongo ametoa Kauli hiyo leo Julai 16, 2024 Jijini Dar es Salaam alipofika makao makuu ya ‘TIC’ ili kukagua utendaji kazi wa kituo hicho na kusikiliza Changamoto inazokikabili.

“Nimefika hapa kwa lengo la kuangalia namna Shughuli zinazofanyika hapa, kwa kweli nimeona na nimeridhishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Uongozi wa TIC kwa kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa Wawekezaji mbalimbali wa ndani na Nje ya Tanzania” amesema.

Previous articleTANZANIA, MAREKANI WASHIRIKIANA KUPAMBANA DHIDI YA UGONJWA WA SARATANI
Next articleRAIS DKT. SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UPANUZI NA UKARABATI KIWANJA CHA NDEGE SUMBAWANGA NA KUZINDUA MIRADI MBALIMBALI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here