Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amekabidhiwa hundi yenye thamani ya shilingi Bilioni 2 kutoka kwa taasisi za umma kwa ajili ya waathirika wa maafa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea wilayani Hanang mkoani Manyara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Desemba, 2023.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla fupi ya upokeaji Hundi ya michango kutoka Taasisi mbalimbali kwa ajili ya Maafa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea Katesh, Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 10 Desemba, 2023.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango akiondoka Ikulu mara baada ya hafla fupi ya kupokea Hundi ya michango kutoka Taasisi mbalimbali kwa ajili ya Maafa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea Katesh, Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 10 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Desemba, 2023.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango akizungumza kwenye hafla ya upokeaji wa hundi ya michango ya Maafa ya mafuriko, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya hafla fupi ya kupokea Hundi ya michango kutoka Taasisi mbalimbali kwa ajili ya Maafa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea Katesh, Ikulu Jijini Dodoma tarehe 10 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Msajili wa Hazina Bw. Nehemia Mchechu pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali, Ikulu Chamwino Mkaoni Dodoma tarehe 10 Desemba, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amekabidhiwa hundi yenye thamani ya shilingi Bilioni 2 kutoka kwa taasisi za umma kwa ajili ya waathirika wa maafa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea wilayani Hanang mkoani Manyara.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Ikulu, Chamwino ambapo Rais Samia amekabidhiwa hundi hiyo kutoka kwa Msajili wa Hazina, Bw. Nehemia Mchechu kwa niaba ya taasisi mbalimbali za serikali.
Aidha, Rais Samia amesema lengo la kuwachangia waathirika hao ni kuweza kuwapatia mahitaji muhimu ili waweze kurejea katika maisha yao ya kawaida.
Hali kadhalika, Rais Samia ameitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kukamilisha tathmini ya maafa hayo kwa waathirika ili serikali ianze mchakato wa kuwarejesha katika makazi rasmi.
Rais Samia amewataka Watanzania kutunza mazingira kwa kusafisha na kuacha kutupa takataka katika mitaro na kuhakikisha inazibuliwa kwa wakati ili mvua zinaponyesha iweze kutiririsha maji.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amezishukuru taasisi za umma, wafanyabiashara na Watanzania kwa ujumla kwa kuonesha mshikamano katika kusaidia waathirika wa maafa hayo.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Taasisi za Umma wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu