Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo wa pili kutoka kushoto akimsikiliza Meneja Masoko na Mawasiliano Shirika la Madini Tanzania STAMICO Bw. Geofrey Meena wakati alipokuwa akimuelezea kuhusu utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Waziri huyo juu ya upandaji wa miti wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya shirika hilo jijini Dodoma, Dkt. Suleiman Jafo leo Septemba 25, 2023 ameshiriki katika zoezi la upandaji wa miti kwenye viwanja vya Maonesho ya teknolojia ya madini yanayoendelea kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita, kushoto ni Waziri wa Madini Bw. Anthony Mavunde na katikati ni Grace Kingalame Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale mkoani humo.
(NA JOHN BUKUKU-GEITA)
……………………………….
Waziri ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Suleiman Jafo amelipongeza Shirika la madini la taifa STAMICO kwa kutekeleza kwa vitendo maagizo aliyoyatoa wakati wa Maadhimisho wa Miaka 50 tokea kuanzishwa kwa STAMICO mwaka jana Agosti 12, 2022.
Wakati wa maadhimisho hayo STAMICO walikuja na Kampeni ya STAMICO na Mazingira at 50! kwa lengo la kuhakikisha pamoja na uendeshaji wa shughuli za uchimbaji wa madini lakini kuhakikisha mazingira yanatunzwa kikamilifu.
“Nawashukuru sana STAMICO kwa kutekeleza kwa vitendo maagizo yangu ya upandaji miti nimeambiwa mpaka sasa mmeshapanda miti 1650 katika Mkoa wa Dodoma na Geita ni jambo zuri sana.”
Mimi nilifanya ziara bila kuwambia kwa kutembelea eneo la ipagala kuona kama kweli mmetekeleza kwa vitendo maelekezo nimekuta kweli mmetekeleza yote kwani niliona mmezungushia uzio na miti inaendelea vizuri sana.” amesema Dkt Suleiman Jafo
Aidha Mhe Waziri ameshukuru Shirika kwa kufanya kazi kwa pamoja na vikundi mbalimbali Kama vile Kikundi cha Wanawake na Samia nimeambiwa mliwapa kazi ya kupanda na kutunza miti hapa EPZA miti 560 na miti hii inazidi kustawi vizuri na mmeenda mbali zaidi na mmeweza kuwapa uwakala ya Kuuza Nishati Mbadala ya Kupikia kwa Mkoa wa Geita, kweli Stamico umeupiga mwingi amesema Mhe Dkt. Jafo.
Katika tukio la upandaji miti jumla ya miti 340 iliweza kupandwa na , Mhe Jafo na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde, Grace Kingalame Kaimu Mkuu wa mkoa wa Geita na mkuu wa wilaya ya Nyang’wale pamoja na viongozi wengine wa chama na Serikali wameshiriki katika shughuli hiyo ya kupanda miti.
Miti hiyo imepandwa katika Viwanja vya Bomba mbili (EPZA) ambako maonesho ya 6 teknolojia ya madini 2023 yanaendelea na wameshiriki watu mbalimbali zikiwemo taasisi za serikali na mashirika
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo wa pili kutoka kushoto akizungumza wakati aliposhiriki katika zoezi la upandaji wa miti kwenye viwanja vya Maonesho ya teknolojia ya madini yanayoendelea kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita, kushoto ni Waziri wa Madini Bw. Anthony Mavunde katikati ni Grace Kingalame Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita na kulia mwenye kofia ni Meneja Masoko na Mawasiliano Shirika la Madini Tanzania STAMICO Bw. Geofrey Meena.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akipanda mti wakati aliposhiriki katika zoezi la upandaji wa miti kwenye viwanja vya Maonesho ya teknolojia ya madini yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili mjini Geita, wanaoshuhudia ni Waziri wa Madini Bw. Anthony Mavunde na kushoto ni Grace Kingalame Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita.
Waziri wa Madini Bw. Anthony Mavunde akipanda mti wakati aliposhiriki katika zoezi la upandaji wa miti kwenye viwanja vya Maonesho ya teknolojia ya madini yanayoendelea kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita wanaoshuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo na Grace Kingalame Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akimwagilia maji mti uliopandwa na Kikundi cha Wanawake cha Samia na Wanawake cha Mkoani Geita kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akishuhudia Meneja Masoko na Mawasiliano wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO Bw. Geofrey Meena na wafanyakazi wenzake wakipanda mti katika viwanja vya Bombambili mjini Geita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akimwagilia maji mara baada ya wafanyakazi wa STAMICO kupanda mti kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita.
Wafanyakazi wa STAMICO wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupanda mti kwenye viwanja vya Bombalimbi mjini Geita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akifurahia jambo na kikundi cha Wanawake na Samia cha mkoani Geita wakati alipotembelea katika banda la STAMICO kwenye maonesho ya Teknolojia ya Madini kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akizungumza jambo na kikundi cha Wanawake na Samia cha mkoani Geita wakati alipotembelea katika banda la STAMICO kwenye maonesho ya Teknolojia ya Madini kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akizungumza jambo na kikundi cha Wanawake na Samia cha mkoani Geita wakati alipotembelea katika banda la STAMICO kwenye maonesho ya Teknolojia ya Madini katika viwanja vya Bombambili mjini Geita kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Shirika la Madini la STAMICO Bw. Geofrey Meena.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akiwa katika picha ya pamoja na kikundi cha Wanawake na Samia cha mkoani Geita wakati alipotembelea kwenye banda la STAMICO kwenye maonesho ya Teknolojia ya Madini kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita