Ofisa Masoko ya nje wa TAN-TRADE Upendo Ndunguru (kulia mwenye fulana nyekundu) akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu kassim Majaliwa (katikati mwenye suti ya bluu) kuhusu Kliniki ya Biashara inazoziunganisha Taasisi zipatazo 13 za Serikali kwenye Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayozishirikisha sekta za madini yanayofanyika Mkoani Geita.
Na: Mwandishi wetu, GEITA.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TAN-TRADE) kufanyakazi kwa pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na halmashauri husika kwenye Kliniki ya Biashara ili kuweza kushughulikia changamoto mbalimbali za Wafanyabiasha hasa katika upatikanaji wa Ardhi na vibali.
Mhe. Waziri Mkuu ameyasema hayo alipokuwa kwenye Kliniki ya Biashara kupata maelezo na kujionea huduma wanazozitoa wakati wa ziara yake ya kukagua mabanda ya wadau mbalimbali kwenye Maonesho ya Nne ya ya Teknolojia ya na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini aliyoyafungua Septemba 22 Mwaka huu Mjini Geita.
Aidha alimweleza kiongozi wa Kliniki hiyo umuhimu wa Wizara ya Adhi na halmashauri kuweo kwenye Kliniki hiyo kutarahisisha upatikanaji wa huduma kwa pamoja na hivyo kutawasaidia wananchi kuweza kupata huduma zote sehemu moja huku akiipongeza TAN-TRADE kwa kubuni kitu kizuri cha kuweza kuwahudumia watu kwa pamoja.
Kwa upande wake Kiongozi wa Kliniki hiyo Ofisa Masoko ya nje wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (TAN-TRADE) Bi. Upendo Nduguru alimshukuru Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa kwa kuweza kuitembelea Kliniki hiyo huku akimueleza kazi wanazozifanaya kuwa ni utoaji wa huduma kwa pamoja kwa wanzanchi ili kutatua changamoto zao kwa wakati sahihi.
Alizitaja Taasisi zinazotoa huduma kwa pamoja kwenye Kliniki hiyo ni pamoja na TAN-TRADE, BRELA, TIA, SIDO, FCC, TRA, TIRA, TIC, EPZA, GS1, NEEC, na Mkeamia Mkuu wa Serikali.
Maonesho hayo ya siku 10 yanatarajiwa kufungwa rasmi Septemba 26 mwaka huu na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.