Na: Stella kessy
KIKOSI cha timu ya Taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 (TANZANITE) kesho kitashuka dimbani kuchuana na Eritrea katika michunao kuwania kufuzu kushiriki Kombe la Dunia.
Mchezo huo utachezwa katika dimba la Chamanzi nje kidogo ya jijini la Dar es Salaaam manira ya saa tisa kamili jioni
Akizungumza na waandishi wa habari leo Kocha mkuu wa timu hiyo Edna Lema amesema kuwa kikosi kimejipanga vyema katika kuhakikisha kinafanya vyema.
“Wachezaji wapo vizuri na sina majeruhi yoyote kila mchezaji amejipanga vyema kuhakikisha wanaitangaza vyema Tanzania lakini pia tumefanyia kazi makosa yetu ambayo walitokea hapo awali” amesema
Aidha kocha Edna amewataka watanzania wote kuzidi kuoimbea timu hiyo na kuipa ushirikiano huku akiwaahidi kwamba kikosi chake kitafanya vizuri kutokana na maandalizi waliokuwanayo.
Naye nahodha wa timu ya Tanzanite Irene Kisisa amesema kuwa mchezo wao wa kwanza dhidi ya Eritrea ulikua mgumu lakini waliweza kufanya vizuri kutokana na maaandalizi mazuri pamoja na kuzingatia mambo yote waliyofundishwa na waalimu wao.
Hata hivyo amewaomba watanzania pamoja na wadau wa soka kuendelea kuwa na imani na kikosi chao kwa kuwa kimejiandaa vyakutosha na kwamba hakitawaangusha katika mchezo wa kesho.
Hii ni mara ya 20 kwa Michuano ya Kombe la Dunia kwa wanawake wa U-20 kufanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000 ikijumuisha nchi wanachama wa FIFA hata hivyo mwaka 2020 michuano hiyo haikufanyika kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa Uviko-19.