Home BUSINESS TASAC KUENDELEA KUIMARISHA USALAMA VYOMBO VYA USAFIRI WA MAJI

TASAC KUENDELEA KUIMARISHA USALAMA VYOMBO VYA USAFIRI WA MAJI

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Kaimu Abdi Mkeyenge akizungumzia na waandishi wa habari (hawamo pichani), wakati wa kuhitimiaha Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane Agosti 8,2023 katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini, Mbeya.

(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kaimu Abdi Mkeyenge, amesema kuwa, Taasisi hiyo, itaendelea kudhibiti usafiri wa vyombo vya maji unaendana na viwango vya Kimataifa katika kutoa huduma Bora na salama.

Mkeyenge ameyasema hayo Jijini Mbeya wakati wa kuhitimiaha Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane, yaliyofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini humo.

Ameeleza kuwa, Mkoa wa mbeya upo kimkakati unaozalisha mazao mbalimbali ikiwemo mchele na Maharage, ambapo wakati mwengine wanatumia usafiri wa maji katika kusafirisha mazao yao kwa kutumia ziwa Nyasa lililopo katika Mkoa huo.

“Tunaendelea kudhibiti usafiri wa vyombo vya maji ambao unaendana na viwango vya Kimataifa katika kutoa huduma”

“Shirika lipo kuhakikisha viwango vya usafiri vinaendana na viwango katika kuleta tija hapa nchini. Natoa wito kwa wamiliki wote wa vyombo vya maji katika Ziwa Nyansa kufata sheria na utaratibu” amesema Mkeyenge.

Previous articleWAZIRI PROFESA MKUMBO ATEMBELEA KIWANDA CHA SAPPHIRE PWANI
Next articleWANNE KUIWAKILISHA TANZANIA CHAGUO LA AWALI FUTURE FACE KIMATAIFA 2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here