Home BUSINESS WATANZANIA TUCHANGAMKIE FURSA KUTOKA IRAN

WATANZANIA TUCHANGAMKIE FURSA KUTOKA IRAN

Na:Neema Adriano

Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE  Bi. Latifa Mohamed Khamis amewaasa Watanzania kuchangamkia fursa za biashara katika nchi ya Iran

Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya Taifa la Iran katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Sabasaba yanayofanyika Katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

“Huu ni wakati Watanzania kubadili uwelekeo kwa kuchangamkia fursa zilizopo Irani hususani katika sekta ya kilimo, afya, teknolojia na elimua Ambapo katika sekta ya kilimo Tanzania tuna fursa za kupeleka Ufuta, ngano na mafuta, ni fursa nzuri ambayo wakulima wetu wanapaswa kuichangamkia ili waweze kunufaika nayo.

“Kwa upande wa Afya pia wenzetu wametuzidi vitu vingi, tumeshafanya maongezi na ubalozi wa Iran hapa nchini na wamekubali kuleta madaktari wao ambao kutakuwa na kambi maalum kubadilishana utaalamu wao na madaktari wetu, teknolojia wanazotumia na sisi basi hatimae tuweze kupiga hatua zaidi katika matibabu.” Amesema.

Hivyo amewataka Watanzania wafikirie Iran kwa ajili ya kufanya nao kazi, vizuri katika suala la huduma kwa wateja, gharama kufanya biashara Irani sio ghali, ni Dola 100 ukibadilisha unapata zaidi ya elfu Hamsini hivyo watanzania wanaweza kwenda kubadili upepo wa kibiashara ili waweze kupata mabadiliko ya kibiashara.

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JULAI 13, 2023
Next articleRC CHALAMILA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUTOA ASILIMIA 10 YA MIKOPO KWA WANAWAKE ,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here