MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila(katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.Mobhare Mtinyi(kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE ) Bi.Latifa Khamis wakati wa ziara ya Mkuu huyo wa Mkoa alipo tembelea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Julai 11,2023.
Akiwa katika viwanja hivyo vya maonesho hayo ya Kimataifa ya Sabasaba RC Chalamila ametembelea baadhi ya mabanda na kujionea bidhaa na shughuli zinazofanywa na Taasisi na Kampuni mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Akiwa katika banda la Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ameshuhudia namna ya utengenezwaji wa mashine mbalimbali unaofanywa na Shirika hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Maonesho hayo RC Chalamila ame mpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusimamia Halmashauri zote nchini kutoa sehemu ya mapato(asilimia 10) kwa ajili ya mikopo ya makundi maalum ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ambao nao wamepata fursa ya kushiriki katika Maonesho hayo.
Maonesho haya ya Biashara ya Kimataifa yalizinduliwa rasmi Juni 28,2023 na yanatarajiwa kufikia tamati Julai 13 mwaka huu ambapo nchi mbalimbali zimeshiriki.
Mwisho.