Na: Stella Kessy.
KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni Boniface Pawasa amewataka Watanzania kuzidi kuiombea timu leo inashuka dimbani dhidi ya Angola katika mashindano ya COSAFA yanayofanyika Durban, Afrika Kusini.
“Mimi ninaomba watanzania wazidi kutuombea kwani maombi ndio kitu kizuri licha ya kuwa tumejipanga vizuri tunaenda kucheza na timu ngumu, pia na sisi tumejipanga kuitangaza vyema nchi yetu katika mashindano haya ambayo kila timu imejipanga vyema kuhakikisha wanafanya vyema”amesema.
Amesema kuwa timu zote zinazokutana ni ngumu hivyo hakuna budi kufanya vyema katika mchezo huo kwani wamejipanga vyema kuhakikisha timu inaibuka na ushindi.
Kikosi hicho kinashuka leo dimbani dhidi ya Angola ambao jana walishinda bao 8 -6 dhidi ya Afrika kusini huku Tanzania wao walishinda bao 2-1 dhidi ya Comoro.