Home LOCAL FEMNET YAENDESHA KONGAMANI LA KUIMARISHA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA MASUALA YA KISIASA...

FEMNET YAENDESHA KONGAMANI LA KUIMARISHA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA MASUALA YA KISIASA BARANI AFRIKA: NAIBU KATIBU MKUU EAC ANENA.


Mbunge wa Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki mhandisi Pamela Maasay ambaye pia ni msemaji wa wanawake wabunge wa jumuiya hiyo akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha.


Rose Njilo mmoja wa wagombea ubunge wa Jimbo la Ngorongoro akiongea na waandishi wa habari katika kongamano la wanawake barani Afrika.

Baadhi washiriki wa kongamano la wanawake barani Afrika wakiwa katika picha ya pamoja

Na: Namnyak Kivuyo, ARUSHA.
 
Naibu katibu Mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki, Mhandisi  Stephen Mlote amesisitiza kuendelea kuhamasisha wanawake Katika kuhimarisha ushiriki wao kwenye masuala ya kisiasa barani Afrika ili kuongeza uongozi wa wanawake katika nchi zilizopo barani humo.

Mahandisi Mlote aliyasema hayo wakati akizindua kongamano la wanawake liliofanyikia jijini Arusha lenye lengo la kuimarisha ushiriki wa wanawake katika masuala ya kisiasa barani Afrika,Mhandis Mlote alisema wanawake wanayo nafasi kubwa  ikiwemo hata katika bunge la EAC zipo nafasi maalumu kwa ajili ya  wabunge wanawake.

“Wanawake hao wanaotoka katika nchi za jumuiya ya Afrika ya mashariki kwani kulikuwa na hofu ya kwamba jinsia ya kike hawana fursa nakuona kuwa EAC ni ya upande wa wanaume lakini sivyo bali ni ya jinsia  zote hivyo ni vyema wakaendelea kuchukua nafasi za uongozi ikiwemo nafasi za kazi,”alisema Katibu huyo.

Kwa upande wake mbunge wa Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki  mhandisi Pamela Maasay ambaye pia ni msemaji wa wanawake  wabunge wa jumuiya hiyo alisema kuwa sababu kubwa za wanawake kutokushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi ni kutokana na misingi ambayo iliyojengwa tayari kwenye jamii jambo linalowafanya baadhi ya wanawake kuwa waoga.

Mhandisi Pamela alieleza kuwa uoga wa kwanza unatokana na athari za mfumo dume uliokuwepo awali hasa kwenye kufikiria kuingia kwenye kuwania nafasi za uongozi na hasa za kisiasa kwasababu wameaminishwa  na katika jamii inaoneshwa kwamba wanawake ni watu ambao hawawezi.

Alieleza kuwa sababu nyingine ni kwamba siasa za Afrika zinahitaji rasilimali fedha na asilimia kubwa ya wanawake ambao wapo kwenye nchi za Afrika bado ni wanawake ambao wapo kwenye vipato vya chini, ni wajasiriamali ambao wakifikiria kujiingiza kwenye siasa waaminu ya kwamba hawatakuwa na vipato vya kutosha kuweza kujitosheleza kufanya kampeni na mahitaji mengine.

Pia Muhandisi Pamela alizungumzia Afrika Mashariki kuwa na Rais mwanamke ambaye ni Rais wa Tanzania Mh Samia Hassan Suluhu ambapo alisema kuwa ni chachu kubwa kwa wanawake wadogo  yaani mabinti kwasababu katika historia hasa Tanzania hawajawahi kuona mwanamke kiongizi hasa kwa nafasi ya juu kama Rais.

“Naamini matendo au vitu ambavyo atavitenda Mh Rais Samia ndivyo vitakavyotengeneza mazingira mazuri zaidi kwa wanawake waliopo nchini Tanzania na hata nje ya Tanzania ili kuweza kuwavutia zaidi na kuonuesha kwamba wanawake wakipewa nafasi wanaweza,” Amesema.

Alifafanua kuwa hiyo kwao ni fursa na mdhani ambao Mh Rais Samia anaweza kukutumia zaidi kuwajengea watoto wa kike ili na wao wengi wenye ndoto za kumtaka kuwa viongizi katika nafasi mbalimbali waweze kufanya vizuri na wasikate tamaa.

pia aliomba waandishi wa habari kuwa funguo ya muhimu  wa kuieleza jamii umuhimu wa jambo lolote ambalo linaweza kusaidia jamii au kuitoa nchi sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa kuwaelimisha kupita vipindi mbalimbali kufahamu fursa zilizopo na kuonesha mwanga.

“lakini pia sisi wanawake viongizi tuliopata nafasi mbalimbali kwenye ngazi tofauti tofauti tunatakiwa tusichezee nafasi hizi bali tuwe mifano kwa wengine, tunatakiwa tufanye vizuri tusiwaangushe ili wakisimama waseme nataka kuwa kama yule lakini tukiwaangusha hata kesho mtu akisimama hawezi kupewa nafasi,”Amesisitiza.
 
Naye  Rose Njilo mmoja wa wagombea ubunge  wa Jimbo la  Ngorongoro  wa nafasi iliyoachwa wazi na Marahemu William ole Nasha  alisema kuwa wanataka kuifahamisha Dunia kuwa wanawake wanaweza kuwa viongizi  ambapo yeye ni mwanamke wa jamii ya kifugaji lakini hakusita  wala kuogopa kugombea kati ya wanaume 17 pamoja na kuwa bado katika jamii za kifugaji kuna dhana kuwa mwanamke hawezi kuongoza.

Alieleza kuwa wakati anashiriki katika kinyang’anyiro hicho jamii ilimuona kama mtu ambaye amekiuka Mila na desturi kwasababu bado mfumo dume  umeshika hatamu kwa jamii hiyo kwani bado wana changamoto kubwa, kazi na safari ya kuelimisha jamii hususan akina baba kwani wanawake angalau kwa sasa wamepata mwamko.

“Nakumbuka wakati nasimama kusema sera zangu  walikuwa wanasema kuwa nafaa ila tatizo ni sababu mimi ni mwanamke kwahiyo bado Mila na desturi zetu hazitutambui sisi wanawake kuwa tunaweza kuwa viongizi bora, amesema Rose Njilo.

Jovitha Mlai ni  mwanachama wa mtandao wa jinsia nchini Tanzania alisema ni vyema wakaangalia  vikwazo vinavyomfanya mtoto wa kike kushidwa kuingia kwenye siasa kwa kuanzia kwenye malezi katika kuwavuta wanaume kuchangia kumjenga mwanamke kuingia kwenye siasa.

“Katika malezi ya nyumbani mume na mke wakiwa vijana wahakikishe wanalea wakijua  yeyote kati yao wanaweza kwenda kwenye siasa na mwanamume anachukua malezi katika kuangalia watoto kwa karibu lakini pia kumuangalia mwenzake kimawazo,kimiundombinu ni vyema wakafika mahali tusaidiane,”alisema  Mlai.

Hata hivyo kongamano hilo limeandaliawa na mtandao wa masiliano na maendeleo ya wanawake Afrika (FEMNET) ambao umewakutanisha wanawake mbalimbali kutoka bara la Afrika lakini pia kuwatumia wanawake wabunge la jumuiya ya Afrika Mashariki kuhamasisha wanawake BARANI Afrika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.


 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here