Home LOCAL RC ARUSHA AELEZA ITAC JUHUDl ZA SERIKALI KATIKA KULETA UTAWALA BORA UNAOZINGATIA...

RC ARUSHA AELEZA ITAC JUHUDl ZA SERIKALI KATIKA KULETA UTAWALA BORA UNAOZINGATIA UWAZI NA UWAJIBIKAJI SEKTA ZOTE

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akifungua Kongamano la kimataifa la uwazi, uwajibikaji na utawala bora (ITAC) kwa niaba ya waziri wa fedha na mipango Dkt Mwigulu Nchemba ambaye pia alikuwa akimwakilisha makamu wa Rais Dkt Philip Mpango.

Baadhi ya washiriki wa kongamano la ITAC wakifuatilia jambo katika kongamano hilo linaloendelea mkoani Arusha
.

Magreth Gudluck Msemo mmoja wa washiriki wa kongamano la ITAC akieleza namna kongamano hilo lilivyowasaidia kujua haki zao kama wananchi

Na: Namnyak Kivuyo, ARUSHA

Serikali ya Jamuhuri ya muunganao wa Tanzania imeweka juhudi katika kuhakikisha  kuwa ngazi zote zinakuwa na utawala bora unaozingatia uwazi na uwajibikaji kwenye mifumo yote na sekta zote.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela wakati akifungua kongamano la  kimataifa wa uwazi, uwajibikaji na utawala bora (ITAC) kwa niaba ya waziri wa fedha na mipango Dkt Mwigulu Nchemba ambaye pia alikuwa akimwakilisha makamu wa Rais Dkt Philip Mpango.

Mongela Alisema kuwa utawala bora, uwazi na uwajibikaji kwenye mifumo na sekta zote unaanzia kwenye bajeti, usimamizi wa matumizi, mapato ya serikali lakini pia kuwa wawazi kwamba wadau wote wawe na uwezo wa kupata taarifa bila urasimu.

“Kwa niaba serikali mheshimiwa makamu wa Rais  amedhirisha kuwa siku zote serikali yetu inaozingatia misingi ya utawala bora kwani imeunga mkono juhudi hizi za wadau  za kuhakikisha kwamba vigezo vya uwazi na uwajibikaji vinazingatiwa,”Amesema Mongela.

Alisema kuwa kwa dhana moja watahakikisha kwamba rasilimali za taifa ambazo viongozi wamepewa dhamana ya kusimamia kwa niaba ya wananchi zinasimamiwa vizuri na wananchi wanaona waziwazi faida ya dhamana hiyo na maendeleo ya nchi kuwagusa moja kwa moja. 

Kwa upande wake CPA Ludovick Utoh mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali mstaafu ambaye ni mkurugenzi wa tasisi ya WAJIBU alisema kuwa madhumuni ya kongamano hilo la siku mbili inatokana na dhana ya uwazi na uwajibikaji katika kuleta makusanyo na matumizi bora zaidi ya fedha za umma kwaajili ya kuletea watu maendeleo.

“Na sisi tasisi ya WAJIBU tunafarijika sana tunapoona kinachofanyika kwani miezi miwili mitatu Rais wetu Mh Samia Hassan Suluhu aliwajulisha watanzania kwamba serika imekopa fedha na akaeleza kwa undani matumizi ya zile pesa na huo ndio uwazi tunataka kuuona katika utendaji kazi wa serikali,” Amesema CPA Utoh.

Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo Magreth Gudluck Msemo alisema kuwa kutokana na majadiliano na ripoti iliyozinduliwa wameweza kujua ni kwanini wananchi wanapaswa kujua nini kinachofanyika katika nchi lakini pia kujua namna gani fedha zinatumika pamoja na kujua haki zao kama mwananchi na wajibu wa kuuliza jambo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here