Na: Stella kessy
KOCHA Mkuu wa simba Pablo Franco leo ameanza na ushindi katika mechi yake ya kwanza baada ya kukiwezesha kikosi chache kuibuka na ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Ruvu shooting katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Ukiachana na ushindi huo mnono, Pablo pia ameiwezesha Simba kupiga Kandanda safi na kuwafanya mashabiki wa tumu hiyo kuibua shangwe hasa kipindi cha kwanza.
Medie kagere alifunga bao la kwanza katika dakika ya 17 baada kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Bernard Morrison.
Kagere aliipatia simba bao la pili katika dakika ya 36 baada ya kumalizia mpira uliopanguliwa na mlinga mlango Mohamed Makaka kufuatia shuti kali la mguu wa kushoto na Kibu Denis.
Hata hivyo kibu Denis aliipatia bao la tatu timu yake katika dakika ya 44 akimalizia mpira wa kisigino uliopigwa na Kagere baada ya shambulizi zuri alilofanya langoni mwa Ruvu.
Katika dakika ya 70 Elias maguli wa Ruvu shooting aliipatia timu yake bao kwa kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na shaban Msala kufuatia Walinzi wa simba kuzembea kuondoa hatari.
Simba nayo ilipatana penati katika dakika ya 72 iliyopigwa na Erasto Nyoni mkwaju huo ulipanguliwa na mlinda mlango Makaka baada ya kibu kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
kocha Pablo Franco alifanya mabadiliko akiwatoa Mzamiru Yassin, kagere, Morrison, Hassan Dilunga, Mohamed Hussen na kuwaingiza Erasto Nyoni, Pape Sakho, Duncan Nyoni, Gadiel Michael, na Yusuph Mhilu