Home SPORTS GHANA, LIBERIA KUUMANA FAINALI ZA CANAF KESHO

GHANA, LIBERIA KUUMANA FAINALI ZA CANAF KESHO

 
Na: Stella Kessy

Ghana na Liberia leo zinakutana katika fainali ya  Michuano ya Soka Afrika  kwa watu wenye Ulemavu (CANAF) inatarajia kufanyika kesho katika dimba la Benjamini Mkapa Dar Es Salaam.

Hata hivyo Ghana ilipata nafasi ya kufuzu fainali baada ya kuitandika mabao 3_1 dhidi ya Angola ,huku Liberia imepata nafasi hiyo baada ya kuichapa bao 1_0 dhidi ya Tanzania katika michezo ya hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo iliyofanyika  juzi kwenye Uwanja huo.

Kwa matokeo hayo nafasi ya mshindi wa tatu Tanzania watamenyana dhidi ya Angola  katika Mchezo utakaochezwa kesho  kwenye uwanja huo.

Naye Rais wa Shirikisho la soka la wenye Ulemavu (TAFF) Peter Sarungi,amesema kuwa anamshukuru mungu kwa jambo la kujivunia licha ya kukosa matokeo mazuri na ni sehemu ya kujifunza.

Amesema kuwa Tanzania ilipata nafasi nyingi lakini ikishindwa  kuzitumua  kwa wakati, hivyo wapinzani wakatumia na kuibuka na ushindi .

“Wapinzani wetu  wna uzoefu na wamechukua makombe matatu na  tuangalie ,hivyo kwa muda uliobakia kocha ataweza kuyafanyia kazi mapungufu ikiwamo ya ushambuliqji na  umaliziajikabla kuelekea kombe la Dunia,” amesema Sarungi.

Previous articleTANZANIA YAKAMATA TANI 356 ZA DAWA ZA KULEVYA
Next articleSERIKALI YA RAIS SAMIA IMEJIPANGA KUIMARISHA SEKTA YA VIWANDA: DKT. HASHIL
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here