Home BUSINESS DKT. BITEKO: JAMII WAUNGENI MKONO WACHIMBAJI MADINI WANAWAKE

DKT. BITEKO: JAMII WAUNGENI MKONO WACHIMBAJI MADINI WANAWAKE


Na: Tito Mselem, Morogoro,

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Tafiti zinaonesha uchimbaji wa madini kwa miaka mingi umekuwa ukifanywa na wanaume kuliko wanawake  ambapo kati ya wachimbaji wadogo wa madini 100, wanawake ni 7 peke yake na kuitaka jamii kuwaunga mkono na kuwatia moyo wanawake wanajitokeza kujiunga katika shughuli za uchimbaji madini.

Waziri Biteko ameyasema hayo alipotembelea mgodi wa madini ya vito uliopo katika kijiji cha Nhalo wilayani Gairo mkoa wa Morogoro ambapo amesema wachimbaji wanawake ni waaminifu hawashiriki katika matukio ya utoroshaji madini. 

Dkt. Biteko amesema kuwa, kipindi cha nyuma wachimbaji wadogo wote nchini walikuwa wanachangia chini ya asilimia 4 kwenye pato la madini lakini kwa sasa wachimbaji wadogo wanachangia zaidi ya asilimia 30 katika pato hilo.

Kufuatia hatua hiyo, Sekta ya Madini inauhakika wa kufikia asilimia 10 ya mchango wake kwenye pato la taifa ifikapo mwaka 2025.

Sambamba na hayo, Dkt. Biteko amesema Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeingia mkataba na Benki mbalimbali nchini ili kuwadhamini wachimbaji wadogo waweze kukopesheka ili wachimbe kwa tija.

Aidha, Dkt. Biteko amewatoa hofu wachimbaji wadogo wa madini ya vito juu ya upatikanaji wa soko la uhakika la madini kutokana na dunia kukumbwa na janga la Uviko-19 lililopelekea soko hilo kuyumba.


Naye, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabiri Makame amempongeza Dkt. Biteko kwa kufanya ziara wilayani Gairo ambapo amesema ujio wa Waziri wa Madini unaenda kuzimaliza changamoto zinazo wakabili wadau wa madini wilayani humo.

“Tunaomba utufikishie salamu zetu kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea maendeleo katika Wilaya yetu ya Gairo, mwambie tunamshukuru sana,” amesema Makame.

Previous articleSPIKA NDUGAI AJIUZULU
Next articleHABARI KUU KUTOKA MAGAZETINI ASUBUHI YA LEO IJUMAA JANUARI 7-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here