Home LOCAL BODI YAPONGEZA UDHIBITI WA UINGIZWAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA DUNI NA...

BODI YAPONGEZA UDHIBITI WA UINGIZWAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA DUNI NA BANDIA MIPAKANI

Mwenyekiti wa Bodi Bw. Eric Shitindi akikabidhi nyaraka za TMDA kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenya.

Wajumbe wa MAB wakipata maelezo toka kwa msimamizi wa kiwanda cha kuzalisha gesi tiba katika hospitali ya Mkoa wa Kigoma Maweni.

Wajumbe wa MAB na Menejimenti wakiwa katika kituo cha forodha cha Manyovu Wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.

Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB) imepongeza utendaji kazi wa TMDA kwa kudhibiti uingizwaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi visivyokidhi vigezo vya ubora na usalama nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA, Bw. Eric Shitindi wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa majukumu ya TMDA katika ofisi za Kanda ya Magharibi, mkoani Kigoma tarehe 06 Machi, 2023.

Bw. Shitindi Amesema kuwa Mamlaka imeimarisha shughuli za udhibiti wa bidhaa nchini ambapo ukaguzi katika soko na vituo vya forodha umeimarishwa. Aidha usimamizi wa uzalishaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na gesi tiba umeimarika hivyo kuwa na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa zilizo bora na salama katika soko la tanzania.

Wakati wa ziara hiyo Bodi hiyo ilitembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambapo RC Kigoma Thobias Andengenya amepongeza ushirikiano uliopo kati ya TMDA na taasisi nyingine za serikali katika mkoa wa Kigoma na kuitaka Mamlaka iendeleze ushirikiano huo ili kulinda afya ya wananchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA BW. Adam Fimbo akitoa maelezo kwa wajumbe wa bodi amesema kuwa Mamlaka imejipanga kuimarisha udhibiti wa bidhaa katika mikoa ya inayopakana na nchi jirani kwa kuongeza wakaguzi na vifaa vya utendaji kazi kwa ofisi zote za kanda.

Katika ziara hiyo MAB imetembelea kituo cha ukusanyaji na ufuatiliaji wa Madhara ya dawa pamoja na kiwanda cha kuzalisha gesi tiba kilichopo katika Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Kigoma- Maweni ambapo bodi hiyo imeridhishwa na utendaji kazi wa Mamlaka katika kupokea, kufuatilia na kudhibiti madhara ya dawa nchini pamoja na kusimamia uzalishaji wa gesi tiba ili kulinda afya ya jamii.

Bodi hiyo pia imepata fursa ya kutembelea kituo cha Damu Salama Mkoa wa Kigoma, bandari ya Kigoma na kituo cha forodha cha Manyovu kilichopo wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma

Ziara hiyo inayolenga kukagua utekelezaji wa majukumu ya TMDA inahusisha mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabor na itahitimishwa tarehe 10 Machi, 2023.

Previous articlePUMA YAWAZAWADIA MITUNGI YA GESI, ‘FULL TANK’ WANAWAKE WENYE ULEMAVU
Next articleSTAMICO YAUNGANA NA WANAWAKE DUNIANI KUSHEREHEKEA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here