Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Uratibu wa shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Chrispin Musiba akiongoza kikao cha Wakurugenzi wa Wizara kwenye Mikakati ya Uwajibikaji wa Kisekta katika mapambano dhidi ya Kifua Kikuu kilichofanyika Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara kwenye Mikakati ya Uwajibikaji wa Kisekta katika mapambano dhidi ya Kifua Kikuu wakifuatilia kikao hicho.
Mshauri Mwelekezi Dkt. Oscar Mukasa akiwasilisha mada katika kikao cha Wakurugenzi wa Wizara kwenye Mikakati ya Uwajibikaji wa Kisekta katika mapambano dhidi ya Kifua Kikuu kilichofanyika Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.
Mratibu wa Uraghibishi na Mawasiliano Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma kutoka Wizara ya Afya Bw. Julius Mtemanji (kulia) akifafanua jambo katika kikako hicho.
Mratibu wa Masuala ya ugonjwa wa Kifua Kikuu na UKIMWI kutoka Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Adela Mpina akieleza jambo katika kikao hicho.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Wakurugenzi wa Wizara kwenye Mikakati ya Uwajibikaji wa Kisekta katika mapambano dhidi ya Kifua Kikuu wamekutana Jijini Dodoma kujadili masuala mbalimbali kuhusiana na ugonjwa wa Kifua Kikuu na namna bora ya kuboresha huduma ya afya.
Kikao hicho kilifanyika Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu kikiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Uratibu wa shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Chrispin Musiba.