Na: Costantine James, Geita.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita Kamishina msaidizi Henry Mwaibambe amewataka wachimbaji wadogo wa madini katika mgodi wa madini Nyakafuru uliopo wilayani mbongwe mkoani geita kuacha tabia ya udanganyifu wa kuidanganya serikali kuwa umeibiwa huku hawajaibiwa.
Kamanda Mwaibambe alisema hayo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo zaidi ya 3000 wa mgodi wa nyakafuru uliopo wilayani mbogwe mkoani Geita na kusema kuwa kuna baadhi ya wachimbaji wadogo wamekuwa wadanganyifu kwa kuidanganya serikali kuwa wameibiwa hasa kaboni, dhahabu pamoja na vitu vingine mbali mbali ndani ya mgodi huo.
“Kuna changamoto kubwa sana ya wizi wa kaboni haiwezi kubwa na mimi wanaoiba kaboni ni watu wanaojua kwa namna moja au nyingine wanajua huu ni dhahabu au sio dhahabu lakini kuna vitu viwili katika wizi wa kaboni ambapo kidogo inashangaza huu wizi ulikua umepugua sasa hivi umejitokeza tena lakini asilimia 98% ya wizi wa kaboni ni wale ambao wamekodi planti na wenye planti naomba zaidi tushilikiane lakini acheni udanganyifu wa kuidanganya serikali kuwa umeibiwa wakati hujaibiwa wapo ambao wanaibiwa kweli tunajua kama polisi lakini wapo wengine huwa hawaibiwi kuna mpango tu wa kuidanganya serikali lakini wale ambao wanaibiwa kweli kweli tutashirikiana nao vizuri” Alisema Henry Mwaibambe kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita.
Hata hivyo kamanda wa Mwaibambe akatoa wito kwa wachimbaji hao kuachana na dhana ya kutenda uhalifu katika maeneo mbali mbali na kukimbilia kwenda kujificha maeneo ya migodi wakizani serikali haiwezi kuwafikia katika maeneo hayo.
“Tumegundua eneo hili usalama ni mkubwa sana lakini ndo maficho makubwa mno ya wahalifu kutoka sehemu mbali mbali wapo walio ua mikoa mbali mbali wako hapa wapo walio baka sehemu mbali mbali wapo hapa kuishi maisha ya amani ndo maisha anayotakiwa kuishi mtanzania kwa sasahivi Rais wetu anasisitiza watanzania waishi maisha ya amani akikosa akose kwa haki sisi tuko imara polisi tuna mtandao hata hapa nyakafuru tupo tutafanya oparesheni mbali mbali na tuanfanya hivyo huwa tunawafuma sana wachache wachache wamefanya matukio katika mikoa mbali mbali Iringa huko amefanya matukio Mbeya, Bukoba huko tuache kujihusisha na uhalifu” Alisema Henry Mwaibambe.
Aidha kamanda wa jeshi la zima moto mkoa wa Geita Kamishina mwandamizi msaidizi Zabron Muhumha alisema kwenye maeneo ya machimbo wanashirikiana sana na Afisa madini mkazi wa katika mkoa wa kimadini wa Mbogwe kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhali ya majanga kwa lengo la kuwalinda wananchi wanaofanya shughuli zao katika mgodi huo ikiwa ni pamoja na kupunguza ajari zinazotokea katika maeneo ya migodini.
“kwa upande wa jeshi la zima moto na uokoaji kwenye maeneo ya machimbo tunashirikiana sana na afisa madini mkazi kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhali kwa watu ambao wanachimba na wanaenda wchini maanayake machimbo yetu mengi yanaenda kina mpaka mita zaidi ya 100 kwa maanaake sisi tunafanya ukaguzi na tayari tumeshapanga na afisa madini wa mbogwe kwamba tutakuja eneo hili kutoa elimu kwa ma insipekita jinsi gani ya kukagua mashimo” Alisema Kamishina mwandamizi msaidizi Zabron Muhumha kamanda wa jeshi la zima moto mkoa wa Geita.