DIWANI wa Kata ya Ilala Saady Kimji akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama ya Mwaka 2022
Mwenyekiti wa CCM mkoa Dar es Salaam Abbas Mtemvu akizungumza na Wanachama wa CCM kata ya Ilala wakati Diwani wa Ilala Saady Kimji alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani (Picha na Heri Shaaban).
Mbunge wa Jimbo la Ilala Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu akizungumza na Wananchi wa Ilala wakati Diwani Saady Kimji alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani (Picha na Heri Shaaban)
Diwani wa kata ya Ilala Saady Kimji akikabidhi zawadi mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM mkoa Dar es Salaam Abas Mtemvu Wakati Diwani Kimji alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani February 11/2023 (Katikati)Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM TAIFA MNEC Simba Juma Gadafi na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde (Picha na Heri Shaaban).
Na: Heri Shaaban (Ilala).
Mwenyekiti wa Chama Cha Màpinduzi CCM mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu, amesema viongozi wa chama cha Màpinduzi CCM waliochaguliwa hivi karibuni walioshindwa kutumikia chama hicho wakae pembeni chama kichague Wanachama wengine .
Mwenyekiti Abas Mtemvu ,alisema hayo kata ya Ilala wakati Diwani wa Ilala alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekekezaji wa Ilani ya Chama ya mwaka 2022 Mpaka 2023 .
“Kuna watu katika chama hichi wameomba uongozi ndani ya chama lakini wanashindwa kutumia nafasi zao naomba wakae pembeni wachaguliwe wengine Ili waweze kufanya kazi .
Wakati huo huo alisema kuhusu ukubwa wa Jimbo la Ukonga la Mbunge Jerry Silaa tumeshauri ligawanywe liwe na majimbo mawili Ili wananchi waweze kupata huduma za Jamii karibu na makazi yao .
Aidha alisema kuhusu ukubwa wa kata pia tutaandika mapendekezo ziwaganywe Ili kila Diwani awe na kata ambayo inamtosha Katika kutumikia wananchi na kufanya kazi za kutatua KERO Ili kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti Mtemvu aliwataka wana Ilala wamtumie vizuri Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mbunge wa Ilala Mussa Zungu katika kujenga Wilaya ya Ilala na kutatua KERO za wananchi na kuleta Maendeleo wote wawe wamoja bila kuchafuana .
DIWANI wa kata ya Ilala Saady Kimji alisema katika kiwasilisha Taarifa za Ilani alifanya Ziara na Wajumbe wa Halmashauri kuu wote kukagua miradi ya Maendeleo walifanya ziara Sharifu shamba Serikali za Mtaa .
DIWANI KIMJI alisema pia walifanya Ziara Barabara ya kisasa Kasongo ,Bungoni ambazo zote zinajengwa kwa kiwango cha Lami .
Aidha alielezea ujenzi wa kituo cha Afya kata ya Ilala ambacho kinajengwa na wadau pamoja na Ubalozi wa Kuwait kata ya Ilala inapata Maendeleo ya haraka .
Aliwataka Viongozi wa chama ,Jumuiya ,waliopo kata ya Ilala kuelezea utekelezaji wa Ilani miradi ya Maendeleo ya Serikali ya Chama Cha mapinduzi unaotekelezwa na Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hasan .
Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa MNEC Juma Simba Gadaf, aliwataka Wana Ilala wajivunie wamtumie vizuri Mbunge wa Ilala Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu Ili Ilala iwe ya kisasa katika Maendeleo .
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde alisema kata ya Ilala ni kata kubwa yenye nguvu ya chama cha Mapinduzi CCM ipo salama amewataka Viongozi wa Chama na Serikali KUJENGA mshikamano kwani CCM inaitaji umoja na mshikamano.
Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungamo Mussa Zungu alisema Diwani Sady Khimji ni Diwani wa mfano amewasilisha taarifa ya utekekezaji wa Chama kwa Viongozi wake wa Halmashauri kuu hivyo waende wakisemee chama pamoja na utekekezaji wa Ilani ya Chama kazi zinazofanywa na Rais .
Mwisho.