Home BUSINESS ORYX GASI YAPELEKA MAFUNZO USALAMA WA GESI MKOANI KILIMANJARO

ORYX GASI YAPELEKA MAFUNZO USALAMA WA GESI MKOANI KILIMANJARO

 


Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Araman Benoite akitoa maelekezo ya namna ya kuwasha moto kwenye jiko la mtungi wa gesi ya Oryx kwa washiriki wa mafunzo ya usalama kuhusu nishati ya gesi ya kupikia yaliyofanyika kwa washiriki 700 kutoka kwenye Wilaya zote saba za mkoa waKilimanjaro.Mafunzo hayo yameandaliwa na Oryx Gas kwa kushirikiana na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Kilimanjaro Shelly Raymond. Mbali ya mafunzo pia kampuni hiyo imekabidhi mitungi 700 na majiko yake kwa viongozi hao wa kata pamoja na wananchi.

Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Araman Benoite akizungumza wakati wa mafunzo yaliyolenga kutoa elimu kuhusu usalama wa gesi na tabia zake kwa washiriki 700 ambao wanatoka katika kata zote za mkoa wa Kilimanjaro ambapo lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha jamii inakuwa salama nakuepukana na madhara yanayoweza kutokea iwapo mtungi wa gesi utatumika vibaya.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakielekezana namna ya kuwasha moto kwenye mtungi wa gesi ya Oryx huku Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Araman Benoite(aliyesimama katikati) akiwa makini kufuatilia.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felichesmi Mramba (wa kwanza kulia) akiwa makini kumsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Araman Benoite (wa pili kushoto) kabla ya kuanza kwa mafunzo ya usalama na kuelewa tabia za gesi kwa yaliyotolewa kwa washiriki 700 katika Mkoa wa Kilimanjaro.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond akizungumza wakati wa mafunzo kuhusu usalama wa nishati ya gesi ya kupikia yaliyoandaliwa na Kampuni ya Oryx Gas Tanzania na mbunge huyo.Jumla ya washriki 700 kutoka kwenye kata zote za mkoa wa Kilimanjaro wameshirikimafunzo hayo sambamba na kupewa mitungi ya gesi ya Oryx pamoja na majiko yake.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo yaliyohusu usalama wa nishati ya gesi ya kupikia majumbaniwakifuatilia maelezo mbalimbali yaliyokuwa yanatolewa na Meneja Masoko wa Oryx Gas Tanzania PeterNdomba(hayuko pichani) alipokuwa akielezea hatua kwa hatua namna ya kutumia mtungi wa gesi yaOryx.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felichesmi Mramba akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro huku akitumia nafasi hiyo kuelezea hatua ambazo zinachukuliwa na Wizara hiyo katika kutekeleza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu kuelekea kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya usalama na uelewa wa tabia za gesi wakiondoka kwenye mafunzohayo wakiwa na mitungi ya Gas ya Oryx ambayo wamepewa bure pamoja na majiko yake lengo likiwa kuhamasisha nishati safi ya kupikia na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa inayoharibu mazingira na afya.

10:Mmoja wa maofisa wa Oryx Gas Tanzania akimtwisha mtungi wa gesi mmoja ya washriki wa mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiweka vizuri mitungi yao baada ya kukabidhiwa na kampuni ya Oryx Gas Tanzania

Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Peter Ndomba akimtishwa mtungi wa gesi mmoja ya wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro baada ya kukabidhiwa mtungi huo pamona na jiko lake.Oryx wametoa mitungi 700 pamoja na majiko yake.

-Pia yakabidhi mitungi ya gesi 700 na majiko yake bure kwa wananchi, viongozi

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

IKIWA ni sehemu ya dhamira yake ya kielimu na sera yake ya Mazingira, Kijamii na Utawala “ESG”, Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Ltd, “OGTL”, imeamua kutoa mafunzo ya nishati ya gesi safi ya kupikia kwa viongozi wa wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro lengo likiwa kujenga ufahamu kuhusu LPG, matumizi yake salama na jinsi kupika kwa kutumia LPG.

Sambamba na mafunzo hayo ambayo yanalenga kuboresha afya ya jamii huku kukilinda mazingira, Oryx pia imekabidhi mitungi ya gesi pamoja na majiko yake kwa viongozi wa ngazi mbalimbali katika kata zote za mkoa wa Kilimanjari na hayo yamefanyika kwa ushirikiano kati ya OGTL na Mbunge wa Viti Maaklum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyoshirikisha washiriki 700 ambao ni wawakiishi wa wananchi kutoka katika wilaya zote saba za Mkoa wa Kilimanjaro, Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Araman Benoite amesema LPG inaweza kuwa hatari ikitumiwa au kutumiwa vibaya. Hata hivyo, ikitumiwa kwa uangalifu na kiwango kinachofaa cha mafunzo na maarifa, Oryx LPG ndiyo nishati safi inayofaa kutumika kwa kupikia.

Ndiyo maana OGTL imeunda miongozo hii ya mafunzo kuhusu matumizi salama ya LPG.

“Matumizi ya LPG yanaendelea nchini Tanzania. Ni wajibu wa wadau wa LPG kuhakikisha Wateja wa LPG wanaelimishwa na kufunzwa kwa njia ambayo wanafahamu kuhusu manufaa yote mazuri ya LPG na jinsi ya kuitumia kwa usalama. Ndio maana Oryx Gas Tanzania imeamua kuzindua mafunzo haya ya usalama kwa watumiaji wake pamoja na elimu ya msingi kuhusu suluhisho la kupikia safi la Oryx LPG.

“Hakuna kitu muhimu zaidi kuliko usalama wa wateja wa OGTL. Hivyo mafunzo ya aina hii yamekuwa kipaumbele sambamba na ukuzaji wa suluhu za Oryx Gas LPG nchini Tanzania. Mafunzo ya aina hii yatatekelezwa hatua kwa hatua kwa jamii zote nchi zima na kwa muda mrefu Oryx Gas Tanzania imeendesha mafunzo kwa makundi mbalimbali ya watumiaji kama vile Super Dealers, Dealers, Retailers.

“OGTL pia imeungana na wadau wakuu kama vile EWURA, Vikosi vya Zimamoto, Wakala wa Uzito na Vipimo ambao wamesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uelewa kuhusu usalama wa LPG kwa wauzaji na wasambazaji. Sasa kampuni ya Oryx Gas Tanzania imeamua kwenda kwenye ngazi ya watumiaji wamwisho, jambo ambalo tunaamini ni jambo sahihi kuelimisha wateja kwa matumizi salama ya LPG huku tukipunguza hatari ya ajali kutokea kwa kukosa maarifa,”amesema Benoite Pamoja na hayo amesema mbali na kutoa mafunzo, vibandiko (Stickers) vya usalama vya LPG hubandikwa kwenye mitungi yote ya Oryx Gas ili kuwakumbusha watumiaji wote kuhusu misingi ya usalama wa LPG.

Akizungumzia majukumu muhimu Benoite amesema wahusika wakuu katika tasnia ya LPG – yaani wazalishaji, wasambazaji, wafanyabiashara, watengenezaji vifaa, na wasafirishaji na hata mafundi -wana majukumu makubwa katika kukuza usalama.“ Sisi sote kama wadau tushirikiane chini ya bendera ya Tanzania LPG Association ili kuhakikisha utekelezaji mzuri wa mpango wa matumizi salama wa LPG,kuendeleza mazoea mazuri na kupiga vita vitendo viovu.

“Mamlaka za kitaifa na za mitaa zinafaa kuchukua fursa ya utaalamu ndani ya sekta ya LPG ili kuhakikisha mbinu za pamoja za utendaji mzuri wa usalama. Wateja wanapaswa kufuata maagizo ya usalama ambayo hutolewa kwao. Kuna wadau wengine wengi, na wote wana jukumu muhimu la kutekeleza.Viongozi na wananchi wataruhusiwa kueneza elimu waliyoipata ufahamu vyema zaidi katika idadi ya watu wa Tanzania.”

Awali Katibu Mkuu wizara ya Nishati Mhandisi Felichesmi Mramba amesema Wizara hiyo inaendelea na mikakati kuhakikisha watanzania wengi wanatumia nishati safi ya kupikia ya gesi na kwa sasa wanaendelea kuzungumza na wabunifu na kampuni kubwa kuangalia uwezekano wa gesi iwe inanunuliwa kama unavyonunuliwa umeme.

Amesema nishati ya kupikia inagusa kila mtu na haiepukiki hivyo ni vema Wizara ya Nishati ikawa na mikakati inayowezesha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia.“Watanzania wengine wamekuwa wamekuwa wakitumia nishati ambayo ina madhara kwa afya na mazingira.”

Aidha amesema nia ni kuona nchi inahama kutoka kwenye nishati chafu ya kupikia na kwenda kwenye nishati safi ya kupikia.Hata hivyo gharama ya kutumia mkaa kwa mwezi mmoja kwa familia ya watu watano ni kubwa zaidi kuliko kutumia mtungi wa gesi.

“Wizara tunafikiria kukutana na wabunifu pamoja na kampuni kubwa za gasi kwa ajili ya kuangaliauwezekano wa gesi iwe inanunuliwa kama vile unavyonunua umeme kwa Luku kupitia simu ya mkononi na hiyo itasaidia kuwezesha wananchi kumudu gharama kulingana na kipato. Tunataka ifike wakri mtu akiwa na Sh.1000 anaweza kununua gesi na akapika , au akiwa na Sh.10,000 basi anunue gesi.” Kwa upande wake Mbunge Shally Raymond amemshukukuru Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania

Araman Benoite kwa kutoa mafunzo hayo mkoani Kilimanjaro sambamba na kutoa mitungi ya gesi na majiko yake bure kwa viongozi wa kata zote za mkoa wa Kilimanjaro huku akisisitiza kuwa Kilimanjaro imeamua kutoka kwenye nishati chafu ya kupikia na kutumia nishati safi ya kupikia ya gesi.

Previous articleMAGAZETI YA LEO ALHAMISI DISEMBA 29 -2022
Next articleRUWASA MKOA WA NJOMBE YATUMIA SHILINGI BILIONI 26.8 KUFIKISHA MAJI KATIKA VIJIJI 95
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Open chat
GREEN WAVES MEDIA
Ahsante kwa kutembeiea ORYX GASI YAPELEKA MAFUNZO USALAMA WA GESI MKOANI KILIMANJARO