Home SPORTS STADE MALIEN 2-1 SIMBA SC

STADE MALIEN 2-1 SIMBA SC

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Klabu ya wekundu wa Msimbazi, Simba SC,  imepokea kichapo cha mabao 2–1 dhidi ya Stade Malien ya nchini Mali, katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Bamako Mali.

Stade Malien walikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za vigogo hao barani Afrika, wakipata  bao la kuongoza dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo, kupitia Taddeo Nkeng.

Katika dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza Stade Malien waliongeza bao la pili lililofungwa na Ismail Simpar, bao lililodumu hadi mapuziko.

kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya ajabu, iliyopelekea SIMBA SC kupata bao katika dakika ya 53 likifungwa na Neo Maema, na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa 2-1.