Maelfu ya Wananchi wamejitokeza na kufurika kumsikiliza Mgombea mwenza wa Urais. kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye mkutano wa Kampeni uliofanyika katika uwanja wa Kigoda, leo Septemba 15, 2025 wilayani Handeni.
Katika mkutano huo, Dkt. Nchimbi amewaomba wananchi wa Wilaya hiyo iliyopo mkoani Tanga, kuipigia kura CCM ili ishinde kwa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.
Katika mkutano huo, Dkt. Nchimbi ameendeleza kampeni, kuomba kura za mgombea urais Dk.Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani.
Dkt.Nchimbi ameanza siku yake ya kwanza mkoani Tanga kufanya mikutano yake ya kampeni za Uchaguzi Mkuu, ambapo mpaka sasa tayari ameshafanya mikutano ya kampeni katika mikoa 11.