Home BUSINESS PURA YAPATA MAFANIKIO MAKUBWA SEKTA GESI ASIIALIA MIAKA MINNE YA Dkt. SAMIA

PURA YAPATA MAFANIKIO MAKUBWA SEKTA GESI ASIIALIA MIAKA MINNE YA Dkt. SAMIA

Mkurugenzi Mkuu wa lMamlaka ya Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Bw. Charles Sangweni akizungumza katika kikao kazi Kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, Jukwaa la Wahariri TEF na PURA kilichofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency Jijini Dar es Salaam Mei 19, 2025.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri akizungumza mapema kabla ya kuanza kwa mkutano huo.fafanua Mambo kadhaa katika kikao kazi hicho.

DAR ES SALAAM.                                                                                      

Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Mhandisi Charles Sangweni, amesema kuwa, katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita, taasisi hiyo imepata mafanikio makubwa katika kusimamia sekta ya mafuta na gesi asilia nchini ikiwa ni matokeo ya usimamizi madhubuti wa Serikali, uwekezaji wa kimkakati, pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa katika kuhakikisha Gesi asilia inapatikana na kuwafikia wananchi.

Mhandisi Sangweni ameyasema hayo alipokuwa akitoa wasilisho katika kikao kazi kati ya PURA na Jukwaa la Wahariri (TEF), chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR), kilichofanyika leo Mei 19,2025 Jijini Dar  es Salaam.

Ameeleza kuwa mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kutolewa kwa leseni ya uendelezaji katika eneo la ugunduzi la Ntorya, hatua inayotarajiwa kuongeza uzalishaji wa gesi asilia nchini, nakwamba uwepo wa ukarabati wa visima vitano vya gesi, umeongeza uimara na ufanisi wa uzalishaji.

“Kampuni za kizawa zimeingia ubia na kampuni za kimataifa katika utoaji wa huduma za kitaalamu na kiteknolojia. Aidha, matumizi ya mifumo ya kidijitali katika shughuli za mafuta na gesi yameongezeka kwa kiwango kikubwa,” amesema Mhandisi Sangweni.

Amebainisha kuwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeimarika katika ukusanyaji wa data za mitetemo kwa ajili ya utafiti wa mafuta na gesi, na limewezesha pia tafiti za awali za kijiolojia, kijiofizikia na kijiokemia—hatua muhimu katika utafutaji wa rasilimali.

Mhandisi sangweni ameeleza kuwa PURA imeongeza ushirikiano wake na taasisi za udhibiti katika ukanda wa Afrika Mashariki. Vilevile, mfumo wa udhibiti wa sekta umeboreshwa kupitia uandaaji na usasishaji wa kanuni na miongozo ya kisheria.

“Majadiliano ya uwekezaji kwa mradi mkubwa wa kuchakata gesi kuwa kimiminika yanaendelea. Pia, idadi ya watumishi imeongezeka kutoka 45 mwaka 2021 hadi kufikia 93 mwaka 2025, hali iliyosaidia kuongeza ufanisi katika usimamizi wa mkondo wa juu wa mafuta na gesi,” amesema,

Kwa mujibu wa takwimu, katika kipindi cha Machi 2021 hadi Machi 2025, Tanzania imezalisha jumla ya futi za ujazo bilioni 301.33 za gesi asilia. Kati ya hizo, futi bilioni 142.35 zilitoka katika kitalu cha Mnazi Bay na bilioni 158.98 kutoka Songo Songo. Hii ni sawa na wastani wa futi bilioni 35.59 kwa mwaka kutoka Mnazi Bay na futi bilioni 39.74 kutoka Songo Songo.

Ikilinganishwa na kipindi cha nyuma, uzalishaji wa gesi umeongezeka, ambapo awali Mnazi Bay ilikuwa ikizalisha wastani wa futi bilioni 32.03 kwa mwaka, huku Songo Songo ikizalisha futi bilioni 25.13 kwa mwaka.

Gesi hiyo imetumika katika matumizi mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa umeme, viwandani, majumbani, taasisi za umma na binafsi, pamoja na kwenye magari.