Home BUSINESS BRELA YATOA MAFUNZO YA MILIKIUBUNIFU KWA WAKUFUNZI JIJINI DAR

BRELA YATOA MAFUNZO YA MILIKIUBUNIFU KWA WAKUFUNZI JIJINI DAR

Na; Lilian Ekonga, DAR ES SALAAM

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA kwa kushirikiana na shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) wameandaa mafunzo ya Miliki Ubunifu yenye lengo la kutoa elimu kwa wakufunzi ili waweze kwenda kuwafundisha watu wengine kwenye masuala mazima ya kulinda bunifu zao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mtendaji Mkuu wa BRELA Godfrey Nyaisa amesema mafunzo hayo yatafanyiaka kwa siku nne kuanzia tarehe 4 mpaka 8 Novemba, ambapo walimu watapewa elimu ya uelewa wa Miliki ubunifu ili wakatoe elimu kwa wengine.

“Bado kuna changamoto ya elimu ya Miliki Ubunifu hivyo BRELA kwa kushiriki na WIPO pamoja na ARIPO tukasema kwamba tuwe na mafunzo kwa hawa walimu kwa maana kwamba watakaokwenda kuwafundisha wengine ili elimu hii iweze kusambaa” amesema Nyaisa

Nyaisa amesema kuwa mafunzo hayo yameshirikisha watu kutoka nchi tofauti Barani Afrika ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Botswana na Malawi, nakwamba anaamini elimu hiyo itasambaa na matokea yataonekana katika jamii ya Tanzania, Afrika na Dunia kwa Ujumla.

Ameongoza kuwa mafunzo hayo  yataisaidia jamii kuwa na ulewa wa kutosha wa kutofautisha Bunifu ambazo hazina sifa na zile ambazo zinahitaji kuboreshwa ili ziweze kuwa na sifa,  na ambazo zina sifa waweze kuzirasimisha,

“Mafunzo haya yanaenda sambmba pia na kutoa elimu kwa majaji hasa wa kesi zinazoenda mahakamani ili waweze kuwa na Elimu ya Miliki Bunifu katika kutatua kesi za aina hiyo ili kutoa hukumu za haki” ameongeza.

Kwa upande wake Makamu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Prof William Anangisye amesema lengo kubwa la mafunzo ya hayo ni kuwafundisha umuhimu wa vile tunavyozalisha ikiwemo tafiti, na ubunifu huo uweze kuzaa matunda na kutpata bidhaa bora kwaajili ya kukuza Biashara.

Naye Wakala wa Usajili Bishara na Mali Zanzibar BPRA , Mohamed Ali Maalimu, amesema wabunifu wengi wana uelewa wa masuala ya  Miliki Ubunifu hivyo uwepo wa mafunzo hayo ni hatua kubwa katika kuhakikisha wabunifu wanalinda kazi zao na kuapata hati miliki zitakazopelekea kufanya kazi zao kwa uhuru..

“Elimu hii itawasaidia kuweza kulinda mali zao na hati miliki pale itakapotokea mtu anataka kutumia kazi ya mtu mwingine”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here