Home LOCAL CHADEMA KANDA YA KASKAZINI KWAFUKUTA, NI MGOGORO WA UONGOZI NDANI YA CHAMA

CHADEMA KANDA YA KASKAZINI KWAFUKUTA, NI MGOGORO WA UONGOZI NDANI YA CHAMA

Taarifa za hivi karibuni kutoka Chadema zinaashiria mvutano wa madaraka kati ya Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, na Katibu wake, Amani Golugwa.
Mgongano huo umeonekana wazi pale ambapo Mwenyekiti wa kanda ameitisha mkutano na waandishi wa habari huku Katibu wa Kanda akıtoa taarifa ya kuanza kwa uchaguzi wa ndani wa chama kanda. Wadau wanahoji  wanafanyaje shughuli ya uchaguzi wa chama katikati ya uchaguzi wa serikali za mitaa?
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Oktoba 23, 2024, uongozi wote wa wilaya ya Longido na mkoa wa Arusha umepigwa chini kwa madai ya utovu wa nidhamu na kwenda kinyume na maadili ya chama. Uamuzi huo umechukuliwa baada ya tukio la Oktoba 22, 2024, ambapo viongozi waliodaiwa kushindwa kusimamia uchaguzi wa ndani kwa haki walihusishwa na vitendo vya kihuni.
Kuvunjwa kwa uongozi huu kunadokeza kuwepo kwa mgongano wa kimkakati kati ya uongozi wa kanda chini ya Godbless Lema na maamuzi kutoka ofisi inayoongozwa na Katibu Amani Golugwa.
Haya yote yanaendelea wakati mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji ukiendelea. Wakati vyama makini vinajiandaa na uchaguzi wao Chadema wanaendeleza migogoro na mivitano ya ndani. 
Ila ni chama hichi hichi kitakapo bagazwa kwenye uchaguzi kitaanza kuilalamikia serikali. Inashangaza pale chama kinapo jiita cha ukombozi na kinashindwa hata kujikomboa chenyewe.
Previous articleMAELFU KUPATA ELIMU YA MPIGA KURA NGORONGORO
Next articleMIAKA MITATU YA RAIS SAMIA MADARAKANI ONGEZEKO LA MAKUSANYO MADINI YAPAA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here