Home BUSINESS WAZIRI JAFO ATAKA WATANZANIA KUJIAMINI NA KUWEKEZA KATIKA VIWANDA NCHINI

WAZIRI JAFO ATAKA WATANZANIA KUJIAMINI NA KUWEKEZA KATIKA VIWANDA NCHINI

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Selemani Jafo (Mb) akioneshwa na Mkurugenzi wa Hill Group Bw. Hillary Shoo jinsi mchakato wa uzalishaji nyama ya kuku wa kisasa kupitia mtambo wa Grader ambao unatumika kupima kilo ya nyama kabla ya kuwekwa kwenye vifungashio alipotembelea Kiwanda cha Hill Farm kilichopo Matimbwa Bagamoyo Pwani Septemba 11, 2024

……..

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo ametoa rai kwa Watanzania kujiamini kuwa wananaweza kuanzisha viwanda na kufanya biashara ili kuongeza ajira, pato la Taifa na uchumi wa nchi.

Vilevile, ametoa wito kwa
Watanzania kupenda kununua na kutumia bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vilivyopo nchini ili kuviwezesha kuendelea na uzalishaji, na kutowavunja moyo wawekezaji.

Dkt Jafo ameyasema hayo Septemba 11, 2024 alipotembelea Kiwanda cha Hill Farm kilichopo Matimbwa Bagamoyo Pwani kujionea shughuli za uzalishaji na kisikiliza na kutatua changamoto zao.

Aidha, Dkt. Jafo amepongeza uwekezaji huo uliofanywa na hill group ambao umesaidia kuleta mapinduzi katika sekta ya uzalishaji nyama ya kuku wakisasa na kutoa wito kwa wadau wengine kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ambayo inatoa mikopo nafuu kwa wawekezaji katika sekta ya kilimo.

Naye Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) nchini Bw. Frank Nyabundege, amewashauri wafanyabiashara na wawekezaji wengine kuwekeza katika viwanda vinavyochakata mazao ya kilimo na mifugo kwa kuwa kuna fursa nyingi za uwekezaji huku akitoa wito kwa wawekezaji hao kuweza kutumia vizuri fedha za udhamini wanazopata kutoka benki hiyo

“ Hapa leo tumeshuhidia uwekezaji wa kisasa ambao pengine Tanzania nzima hakuna katika sekta ya uzalishaji nyama ya kuku wa kisasa , hivyo nitoe pongezi kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kuwashika mkono wawekezaji pamoja na Rais wetu ambae ametoa zaidi ya bilioni 100 kwa wawekezaji, nitoe wito kwa wadau wengine kuja Benki ya Maendeleo ya kilimo” Bw. Frank Nyabundege,

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Makampuni ya Hill Group Bw. Hilary Shoo, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwapa mazingira wezeshi ya kufanya biashara na uwekezaji huku wakipata msamaa wa kodi mbalimbali kutoka Serikalini na TADB kwa mkopo wa gharama nafuu

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Selemani Jafo (Mb) akioneshwa na Mkurugenzi wa Hill Group Bw. Hillary Shoo jinsi mchakato wa uzalishaji nyama ya kuku wa kisasa kupitia mtambo wa Grader ambao unatumika kupima kilo ya nyama kabla ya kuwekwa kwenye vifungashio alipotembelea Kiwanda cha Hill Farm kilichopo Matimbwa Bagamoyo Pwani .

2.Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Selemani Jafo (Mb) akiangalia chumba maalumu uchakatati wa mabaki yanayotokana uzalishaji wa nyama ya kuku ambayo hutumika kutengenezea chakula cha mifugo mingine kama kuku na nguruwe alipotembelea Kiwanda cha Hill Farm kilichopo Matimbwa Bagamoyo Pwani Septemba 11, 2024

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here