Home BUSINESS WAWEKEZAJI NCHINI WATAKIWA KUKATA BIMA YA BIASHARA

WAWEKEZAJI NCHINI WATAKIWA KUKATA BIMA YA BIASHARA

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Kaimu Mkeyenge, amewataka wawekezaji nchini kukata bima za biashara ili kuepuka hasara zitokanazo na majanga.

Mkeyenge alitoa rai hiyo jana Julai 9, 2024 jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea banda la NIC lilipo kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimaamtaifa (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.

Mkeyenge alisema kwasasa uwekezaji umeongezeka nchini hivyo ni muhimu wafanyabiashara na wamiliki wa kampuni kuzingatia kukata bima kubwa ili mali zao kuwa na uhakika wa salama.

Alisema wanatoa bima za maisha na bima sizizo za maisha ambapo bima zisizo za maisha zinaenda moja kwa moja na kauli mbiu ya maonesho hayo isemayo ‘Tanzania Mahali Salama Pa Biashara na Uwekezaji’.

Mkeyenge alisema pamoja na kuwa ni taasisi ya serikali lakini pia wanafanyabishara kwasababu wana jukumu la kulipa kodi na kuwahudumia Watanzania.

Akizungumzia mikakati waliojiwekea katika mwaka mpya wa fedha, alisema Watanzania wengi hawana uelewa wa bima hivyo litakuwa jukumu kubwa la kuendelea kuelimisha umma.

“Kutoa uelewa kwa wananchi kwa kuwafuata walipo na kuwapa elimu ya Bima ili kuongeza idadi ya wanaojiunga na bima,” alisisitiza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here