Home LOCAL RAIS SAMIA KUMPOKEA RAIS NYUSI WA JAMHURI YA MSUMBIJI

RAIS SAMIA KUMPOKEA RAIS NYUSI WA JAMHURI YA MSUMBIJI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kumpokea Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi tarehe 02 Julai, 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Nyusi anatarajia kuwasili nchini leo jioni ambapo atafanya Ziara ya Kiserikali ya siku tatu.

Rais Samia na mgeni wake Rais Nyusi watashiriki mazungumzo ya pamoja ambayo yatajikita katika sekta ya biashara, uwekezaji, ulinzi na usalama na kisha kushuhudia uwekaji saini wa makubaliano katika sekta mbalimbali za ushirikiano.

Ziara hii itaendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria, kidugu na kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji ambao uliasisiwa na viongozi wetu; kiongozi wa kwanza wa chama tawala cha nchi hiyo (FRELIMO), Hayati Eduardo Chivambo Mondlane na Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere.

Rais Nyusi pia anatarajia kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) siku ya tarehe 03 Julai, 2024 ambapo ataambatana na mwenyeji wake Rais Samia.

Rais Nyusi ataondoka nchini tarehe 04 Julai, 2024.Sharifa B. NyangaKaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Previous articleNHC YATEKELEZA MRADI WA SAMIA HOUSING SCHEME KWA MAFANIKIO MAKUBWA
Next articleMNDOLWA AHIMIZA WATUMISHI WA NIRC KUZINGATIA UBORA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA SERIKALI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here