Home BUSINESS PPRA YAWAPA KIPAUMBELE WAZAWA ZABUNI ZOTE KUANZIA BIL. 50

PPRA YAWAPA KIPAUMBELE WAZAWA ZABUNI ZOTE KUANZIA BIL. 50

MAMLAKA ya Udhibiti na Manunuzi ya Umma (PPRA) kupitia sheria mpya imewapa kipaumbele wazawa zabuni zote za kuanzia Bilion 50 kushuka chini ziende kwa wazawa.

PPRA wameanza matumizi ya sheria mpya ya ununuzi Sheria namba 10 ya mwaka 2023 na kanuni zake kulingana na tangazo la Serikali namba 518 lililochapishwa Juni 25 2024.

Hayo yamesemwa Julai 8,2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Tafiti Maendeleo na Ubunifu wa Mamlaka wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Mhandishi Masunya Nashoni alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika maonesho ya 48 ya Biashara Sabasaba.

Amesema sheria hiyo mpya imekuja kwa kuwaangalia zaidi wazawa kwa kutoa upendeleo kuanzia kifungu namba 56 hadi 64 sheria hiyo inasema kuwapa upendeleo makundi matatu lile la vijana,wanawake, wazee na watu wenye mahitaji maalum.

Sheria hiyo imeelekeza kila taasisi nunuzi Serikali itenge asilimia 30 ya bajeti kwa ajili ya kuyawezesha makundi hayo kushiriki katika zabuni za serikali.

Amesema wazawa watapewa upendeleo kwa zile zabuni za manunuzi kwa bidhaa za ndani zinazozalishwa ndani iwe malighafi au zingine.

Hivyo Serikali kupitia PPRA inaanza kutoa mafunzo kuwajengea uwezo juu ya mfumo mpya wa ununuzi ya umma kwa mfumo wa kielektoniki, kanuni wa sheria za manunuzi

Mfumo huo umeanza Oktoba 1 mwaka jana tayari taasisi nunuzi 1147 na wazabuni zaidi ya 22000 ambao tayari wameshajiandikisha katika mfumo.

Previous articleBoT YAJA NA KAMPENI KABAMBE ‘ZINDUKA, USIUMIZWE, KOPA KWA MAENDELEO
Next articleNMB YATETA NA WAFANYABIASHARA WANAWAKE WANAOSHIRIKI SABASABA 2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here