Home SPORTS NELSON MANDELA MARATHON KUHAMASISHA MASOMO YA SAYANSI KWA WASICHAN

NELSON MANDELA MARATHON KUHAMASISHA MASOMO YA SAYANSI KWA WASICHAN

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo katika picha) wakati alipokuwa akitambulisha mbio za masafa marefu za Nelson Mandela (Nelson Mandela Marathon) zinazotarajiwa kufanyika September 22, 2024 katika kampasi ya Tengeru Arusha.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Nelson Mandela Marathon Prof. Liliane Pasape kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo katika picha) wakati wa mkutano na vyombo vya Habari Julai 2 , 2024 wakati wa kutambulisha mbio za masafa marefu za Nelson Mandela zinazotarajiwa kufanyika September 22, 2024 katika kampasi ya Tengeru Arusha.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula (Katkati) akijadiliana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Prof. Liliane Pasape (kushoto) na Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Nelson Mandela Marathon Bw. Marco Mwenda (kulia) mara baada ya mkutano na vyombo vya habari kuhusu ujio mbio za masafa marefu za Nelson Mandela zinazotarajiwa kufanyika September 22, 2024 katika kampasi ya Tengeru Arusha.

……..

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela imetangaza ujio wa mbio za masafa marefu za Nelson Mandela zenye kauli mbiu “Stride for Science, Step for Success” (Jitihada kwa Sayansi na Hatua kwa mafanikio) zitakazofanyika Kampasi ya Tengeru jijini Arusha Septemba 22, 2024 .

Akizungumza katika mkutano na Vyombo vya Habari Julai 2, 2024 Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula ameeleza kuwa, lengo za mbio hizo ni kuhamasisha wasichana na wanawake kusoma masomo ya Sayansi,Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na ubunifu katika ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu.

Ametoa wito kwa wadau mbalimbali wakiwemo wanariadha, vyuo vikuu, mashirika binafsi na umma pamoja na kampuni kujumuika pamoja na taasisi hiyo katika kufanikisha mbio hizo, ili kuchangia maendeleo ya elimu hususani kwa masomo ya sayansi kwa wasichana na wanawake ili waweze kushiriki kikamilifu katika kutatua changamoto inayoikabili jamii na viwanda.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Nelson Mandela Marathon Prof. Lilian Pasape amesema maandalizi yanaendelea vizuri na anapenda kuwakaribisha wadau wa michezo kote nchini, hususani watoa huduma kujumuika na taasisi hiyo katika kufanikisha mbio hizo.

Mbio za masafa marefu za Nelson Mandela ambazo zitahusisha mbio a umbali wa Km 5, 10 na 21 zinafanyika kwa mara ya kwanza kwa ada ya ushiriki ya sh. 35,000 inayolipwa kupitia M-PESA 54284944, ambapo baada ya malipo mshiriki atutuma taarifa zake kupitia namba 0756817072 au 0655208508 , malipo hayo yatamuwezesha mshiriki kupata fulana na medali.

Previous articleRAIS SAMIA NA VIONGOZI WA CCM KATIKA HAFLA YA CHAKULA CHA MCHANA NA MGENI WAKE RAIS NYUSI WA MSUMBIJI
Next articleKIWANDA CHA MSD IDOFI CHAZALISHA ZAIDI YA JOZI MIL. 2 ZA GLOVES TOKA KUANZA UZALISHAJI 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here