DAR ES SALAAMÂ
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kupitia Bodi yake ya Bima ya Amana (DIB) imeongeza kiwango cha fidia kutoka shilingi Milioni 1.5 mpaka Milioni 7.5 kitakachotumika baada ya Benki kuanguka.
Aidha kwa sasa kiasi cha juu cha fidia kinachotumika ni Shilingi Milioni 7.5 kilichoanza kutumika mwezi Februari mwaka 2023 ikiwa ni ongezeko la kiwango cha awali cha milioni 1.5.
Hayo yamebainishwa na Afisa Benki wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Twaiba Juma wakati wa mahojiano na waandishi wa Habari kwenye maonesho ya 48 Biashara ya kimataifa (Sabasaba), yanayoendelea kwenye viwanja vya Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es salaam, ambapo amesema toka waongeze kiwango hicho hakuna Benki yoyote iliyofilisika nakwamba zimeendelea kuwa imara.
“Sasa hivi kiwango hicho bado hakijaanza kutumika kutokana na kwamba Benki bado ziko imara katika Sekta ya fedha, na Benki Kuu akiendelea kufanya majukumu yake ya kusimamia Sekta hiyo kwa ufasaha zaidi” ameeleza Twahiba.
Amesema kuwa Bima hiyo inatolewa wakati Benki Kuu ya Tanzania inazifutia leseni Taasisi hizo, na kuichagua Bodi kuwa mfilisi, ambapo inakuwa na jukumu la kulipa fidia kwa wateja pale Benki au Taasisi ya fedha imefilisika.
Amesema kwasasa kiasi cha juu cha fidia kinachotolewa ni Milioni 7.5 ambacho kimeanza kutumika mwezi Februari mwaka 2023 ikiwa ni ongezeko kutoka kiwango cha awali cha milioni 1.5 ambapo tokea kiwango hicho kiongezwe hakuna Benki yoyote iliyofilisika kwani Benki zimeendelea kuwa imara katika sekta ya fedha, na Benki Kuu akiendelea kufanya majukumu yake ya kusimamia sekta hiyo kwa ufasaha zaidi.
Amebainisha kuwa hivi sasa kuna Benki ambazo zipo kwenye ufilisi katika kiwango cha zamani cha Milioni 1.5Â na kuwasihi wateja ambao Benki zao zimefilisika kujitokeza kuchukua stahiki zao, ambayo ni fidia ya amana katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dodoma na Dar es Salaam.
Ametoa mwito kwa waliokopa kwenye Benki ambazo zimefilika hapa nchini kwenda kwenye bodi hiyo ili wapate taratibu za kurudisha mikopo hiyo.
Amezitaja Benki zilizofilisiwa ambazo wateja wake wanatakiwa kwenda BoT kuchukua fidia zao ni EFATA, Njombe Community Bank, Convent Bank, FMB Bank, Kagera Farm Cooperative Bank, Mbinga Community Bank na Meru Community Bank. Â