Home LOCAL OSHA YAELEZA MAFANIKIO YAKE MIAKA MITATU YA Dkt. SAMIA

OSHA YAELEZA MAFANIKIO YAKE MIAKA MITATU YA Dkt. SAMIA

DAR ES SALAAM 

Mtendaji Mkuu wa WAKALA wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, taasisi hiyo imeweza  kusajili zaidi ya sehemu za kazi 11,000 jambo ambalo linatoa tafsiri kuwa kuna mabadiliko chanya ya kiuwekezaji.

Amesema wakati Rais Samia anaingia madarakani OSHA ilikuwa imesajili sehemu za kazi 360 katika maeneo mbalimbali, na kwamba ongezeko hilo ni mafanikio makubwa katika kuimarisha huduma zao kwa wafanyakazi.

Mwenda ameyasema hayo wakati wa mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa na OSHA kwa ajili ya wahariri wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), zaidi ya 50 yaliyofanyika April 19,2024 Jijini Dar es Salaam, yenye lengo la kuwajengea uelewa ili kujua majukumu ya taasisi hiyo na kusaidia kuhabarisha umma kwa ufasaha.

“Tumewaita wahariri ili wajue OSHA inafanya nini, kwanini serikali ilianzishwa, kwani usalama na afya mahali pa kazi, tunaamini wakielewa na kuongea, tunakuwa tumeongea sisi. Kundi hili linakutana na waajiri na wafanyakazi, hivyo kupitia mafunzo haya ya mara kwa mara ni imani yetu kutakuwa na mabadiliko chanya,” amesema.

Amesema mafunzo hayo yamejikita katika sheria ya usalama na afya mahali pa kazi, vihatarishi vya sehemu za kazi na maeneo mengi ambayo yanahusiana na eneo lao.

Mwenda amesema taasisi hiyo pia itajipanga kuhakikisha wahariri na waandishi wa habari wanapata nafasi ya kutembelea maeneo ambayo yamesajiliwa ili kuona mambo ambayo wanayakagua.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule akizungumza alipokuwa akifungua rasmi mafunzo hayo, mesema OSHA imekuwa ikifanya vizuri katika kutekeleza majukumu yake, ila inapaswa kuongeza kasi katika kuhakikisha.

“Tumeona kasi ya wawekezaji kutoka nje na ndani kuwekeza nchini, ila uwekezaji huo utakuwa na tija iwapo sheria, kanuni na taratibu za usalama na afya mahali pa kazi zitazingatiwa na wawekezaji hao na hilo linaweza kuonekana iwapo OSHA itatekeleza majukumu yake kwa weledi,” amesema.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan anapambana kila kukicha kuweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji, lakini haitakuwa na maana iwapo kutakuwa na ukiukwaji katika eneo la usalama na afya mahali pa kazi

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF, na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jukwaa hilo, Salim Said Salim amsema Jukwaa hilo litaendelea kushirikiana na na taasisi hiyo katika kuuhabarisha Umma, na kwamba watakuwa mabalozi wa OSHA kwani mafunzo hayo yamekuwa na manufaa makubwa kwao. 

Mwisho.

Previous articleKAMPUNI YA DRAFCO, PREMATURE BABIES WAELIMISHA ZAIDI YA WATU 700, WATOA MSAADA WA TAULO HOSPITALI YA AMANA
Next articlePITIA VICHWA VYA SOMA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO APRILI 21-2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here