Home BUSINESS BENKI KUU YATOA UFAFANUZI ONGEZEKO WA RIBA MPYA

BENKI KUU YATOA UFAFANUZI ONGEZEKO WA RIBA MPYA

Na: Mwandishi

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa ufafanuzi juu ya ongezeko la riba ya Benki hiyo ya asilimia sita kuwa ni kudhibiti mfumuko wa bei.

Ufafanuzi huo umetolewa na Mkurugenzi wa Utafiti wa Sera na Uchumi wa Benki Kuu, Dk. Suleiman Missango katika kikao na waandishi wa Habari kilichofanyika leo Aprili 8,2024 Jijini Dar es Salaam.

Amesema mwenendo wa uchumi wa Dunia ulikuwa unaashiria uwepo wa mfumuko wa bei hivyo ikaona iongeze riba kutoka asilimia 5.5 hadi asilimia sita katika robo ya pili kuanzia Aprili mwaka huu.

“Wengi walijua tunakwenda kuweka ukomo wa riba sio kweli, kwa kupandisha riba hiyo maana yake tunapunguza ukwasi katika mzunguko na hivyo kudhibiti mfumuko wa bei kwa siku zijazo.

“Kupanda kwa riba hiyo kumezingatia ukuaji wa uchumi , maamuzi mengine yatachukuliwa Julai mwanzoni na riba hii ni ya robo ya kwanza ya Aprili, mwaka huu na inaweza kupungua au kuongezeka kwa kadri ya uchambuzi utakavyokuwa,” amesema Dk.Missango.

Ameongeza kuwa tangu Benki Kuu ianzishe mfumo wa riba hiyo mwaka huu badala ya mfumo wa zamani wa ujazi wa fedha na kwamba hali imeendelea kuwa tulivu na mapokeo yamekuwa mazuri kwa wadau.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here