Home BUSINESS PROF. MKUMBO: NENDENI MKASIMAMIE MASILAHI YA NCHI

PROF. MKUMBO: NENDENI MKASIMAMIE MASILAHI YA NCHI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Raisi, Mipango na Uwekezaji, Professa Kitila Mkumbo (Mb), akizungumza alipokuwa akifunga rasmi kikao kazi cha siku tatu kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na wajumbe wa Bodi na wakurugenzi wa Mashirika ambayo Serikali inamiliki hisa chini ya asilimia 50, Machi 15,2024 Kibaha, Mkoani Pwani. 

Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida akitoa neno kwa wajumbe wa mkutano huo alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi Mkutano huo.

Msajili wa Hazina Nehemiah Mchuchu, akizungumza alipokuwa akitoa neno la utangulizi kuelezea kilichofanyika katika siku tatu za Mkutano huo Kibaha Mkoani Pwani.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Msajili wa Hazina Amon Nnko, akiwasilisha maazimio ya Kikao hicho.

Na: Hughes Dugilo, KIBAHA 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Raisi, Mipango na Uwekezaji, Professa Kitila Mkumbo, ameagiza Bodi zinazowalilisha Serikali kwenye mashirika zenye hisa chache kusimamia kwa ukamilifu mashirika hayo kwa maslahi mapana ya Taifa.

Prof. Mkumbo ametoa maelekezo hayo Machi 15,2024 Kibaha Mkoani Pwani, alipokuwa akifunga kikao kazi cha siku tatu, kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na wajumbe wa Bodi na wakurugenzi wa Mashirika ambayo Serikali inamiliki hisa chini ya asilimia 50.

Alisema kuwa yapo mambo ambayo serikali inawataka viongozi hao kuhakikisha wanayasimamia ili kuleta tija kwa Serikali na Taifa kwa ujumla.

Waziri huyo alieleza kuwa moja ya mambo ambayo Serikali inatamani kuona yanafanyika kwa Kampuni hizo, ni kuona zinawekeza nchini kwani zipo hapahapa.

“Mna nafasi ya kuhakikisha kwamba Makampuni haya yanawekeza Tanzania na kuendana na mazingira ya hapa nchini.

“Utakuta Kampuni kubwa Kutoka nje imewekeza nchini, lakini mazingira yao na namna wanavyoendesha Kampuni kama wapo kwao” amesema Prof. Mkumbo.

Aliwataka viongozi hao kuwa na tabia njema na kuona ujuzi na mbinu ambazo zinazotumika kuhakikisha Kampuni zao zinafanikiwa.

Professa Mkumbo amewataka viongozi hao kutoa mrejesho kwa Serikali ambayo wanaiwakilisha kwa tutoka taarifa za mambo mbalimbali katika makampuni yao.

“Serikali imeamua kuijenga na kuikuza Sekta binafsi katika nchi yetu ili itusaidie, na ukiangalia makampuni mnayofanyia kazi mengi ni Sekta Binafsi, hivyo kusimamia na kufanya kazi kwa weledi ili kuisaidia Serikali kufikia malengo yake” amesema Prof. Mkumbo.

Ofisi ya Msajili wa Hazina iliwaketisha pamoja wajumbe wa Bodi na  wakurugenzi wa Mashirika ambayo Serikali inamiliki hisa chini ya asilimia 50 katika kiikao kazi cha siku tatu, Kibaha, Pwani kwa lengo la kuzungumza nao na kuwakumbusha matarajio ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kusimamia masilahi ya Taifa.

Previous articleAZAKI ZATOA MAPENDEKEZO 9 DIRA YA MAENDELEO 2050
Next articleU.S. CDC NA THPS WAKABIDHI VIFAA NA JENGO JIPYA LA TIBA NA MATUNZO KWA WAVIU USHETU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here