Home BUSINESS WATANZANIA WAASWA UTEMBELEA HIFADHI YA KITULO

WATANZANIA WAASWA UTEMBELEA HIFADHI YA KITULO

Na: Mwandishi Wetu Makete

AFISA Mhifadhi mkuu wa Kanda ya Kusini Jonathan Kaihura Ametoa wito Kwa watanzania kujenga tabia ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo katika hifadhi zetu hapa nchini na hasa hifadhi ya Taifa ya kitulo iliyopo katika mikoa ya Njombe wilayani Makete. Na Mkoa wa Mbeya wilaya ya Rungwe na mbeya vijijini

Amesema kuwa mara zote pamekuwa na dhana ya kwamba wanaopaswa kutembelea na kufanya utalii ni wageni kutoka nie ya Tanzania jambo ambalo si sawa hivyo nivema wakajenga tamaduni ya kufanya utalii kwenye hifadhi mbalimbali hapa nchini .

Kaihura ametoa wito huo Leo January 22 ,2024 wilayani makete wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambao wamejikita katika hifadhi ya Taifa ya kitulo Kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika hifadhi hiyo.

Akizungumzia hifadhi ya Taifa ya kitulo Amesema hifadhi hiyo ilianzishwa rasmi mwaka 2005 na kwamba ni Moja ya hifadhi muhimu ambayo inapatikana nyanda za juu kusini ambapo imezungukwa na mikoa miwili ambayo ni Njombe na Mbeya

Amesema kuwa hifadhi ya kitulo inavivutio vya kustajaabisha Saba, huku akitolea mfano uwepo wa Waterfall ambayo Maji yanatirirka msimu mzima, lakini pia Kuna bustani nzuri sana ya maua ambayo ni uoto wa asili lakini kubwa kuliko mandhari yake ni ya kipekee

“Hapa kitulo hakika Mungu ni wa ajabu sana na amepapendelea sana nadhan mmeona pale kwenye chanzo ambapo Maji yanatiririka msimu mzima na pamepewa jina la Mwakitelima ambaye ndiye alikuwa Mhifadhi mkuu wa kwanza katika hifadhi hii ya kitulo “Amesema Kaihura

Ameongeza kuwa licha ya chanzo hicho lakini pia Kuna maporomoko ya msitu wa mto Nhumbe yote hayo yanapatikana katika hifadhi ya Taifa ya kitulo hivyo watanzania waje kutembelea vivutio hivyo watafurahi na wataburudika.

Amefafanua kuwa hata gharama za kuingia kwenye hifadhi hiyo ni rafiki sana na hata sehemu za maradhi gharama zake ni rafiki sana ambapo kulala katika nyumba zilizopo kwenye hifadhi usiku mmoja ni sh.29000 tu lakini pia huduma za chakula vinywaji vyote vinapatikana ndani ya hifadhi

Pia amesema ndani ya hifadhi hiyo pia Kuna wanyama kama swala na wanyama wengine lakini Kwa upande wa maua Kuna aina 45 za maua lakini pia Kuna mimea aina mbalimbali inapatikana hivyo ni fursa azmu Kwa watanzania kuendeleza kuunga mkono juhudi za Rais DKT. Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vilivyopo nchini Tanzania.

Hifadhi ya Taifa ya kitulo ipo mita 2900 kutoka usawa wa bahari na inazunguka katika mikoa miwili ambayo ni mkoa wa Njombe katika Wilaya ya Makete lakini pia katika mkoa wa mbeya na hasa mbeya vijiji pamoja Wilaya ya Rungwe .Mhifadhi mkuu wa kwanza wa hifadhi hiyo alikuwa anaitwa Simon Mwakilema .

Previous articleDkt. KIDA: SERIKALI IMEONDOA ONDOA TOZO ZAIDI YA 374 SEKTA YA UWEKEZAJI
Next articleBENKI YA CRDB KANDA YA MAGHARIBI YAZINDUA KAMPENI YA AMKA NA CRDB MTAANI KWAKO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here