Home BUSINESS WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA BANDA LA TANZANIA COMMERCIAL BANK MIAKA 50 CHUO...

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA BANDA LA TANZANIA COMMERCIAL BANK MIAKA 50 CHUO CHA USTAWI WA JAMII DAR

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Tanzania Commercial Bank, alipotembelea Banda la Taasisi hiyo katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, yaliyofanyika Disemba 18,2023 Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa  (wa pili kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Kariakoo Bw. Faraji Basso, (kushoto) wakati Waziri Mkuu alipotembelea Banda la Taasisi hiyo, kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, yaliyofanyika Disemba 18,2023 Jijini Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kukua kiuchumi kwa kuchangamkia fursa za mikopo zinazotolewa na Taasisi za fedha zikiwemo Benki.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo alipotembelea Banda la Tanzania Commercial Bank katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, na Wiki ya Ustawi wa Jamii, iliyoenda sambamba na uzinduzi wa vipindi vya Malezi, Makuzi na maadili kwa vijana, iliyofanyika Disemba 19,2023 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha  Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa alisema kutokana na changamoto za kiuchumi familia nyingi zinashindwa kupata muda wa kutosha kulea watoto na vijana ambao ni muhimu katika ujenzi wa Taifa la sasa na baadaye, hivyo mada hiyo ni kengele ya amshaamsha kwa kila mtendaji na mwanajamii kutambua kuwa suala la malezi na makuzi ya watoto na vijana ni msingi wa maendeleo ya Taifa letu.

Katika tukio hilo, Tanzania Commercial Bank walishiriki wakiwa ni wadhamini wa maadhimisho hayo.

Hatua hiyo ni katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya kuhakikisha makundi mbalimbali ya kijamii yanaendelea kunufaika kiuchumi, nakwamba Tanzania Commercial Bank imeendelea kuwa mdau mkubwa kwa kuweka mazingira wezeshi yakiwamo huduma za mikopo itakayosaidia kuchochea maendeleo ya wanawake, makundi mbalimbali na watanzania wote nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here