Home LOCAL WANANCHI KATESH WAISHUKURU SERIKALI KWA MSAADA WA KIBINADAMU

WANANCHI KATESH WAISHUKURU SERIKALI KWA MSAADA WA KIBINADAMU

Matukio Katika Picha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akigawa vifaa vya msaada wa kibinadamu kwa waathirika wa poromoko ya matope kutoka Mlima Hanang’

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amesema misaada yote inayotolewa na wadau mbalimbali itawafikia walengwa walioathirika wa poromoko ya matope kutoka Mlima Hanang.

Kauli hiyo ameitoa wakati alipozindua zoezi la ugawaji wa vifaa vya msaada wa kibinadamu kwa familia 205 zilizoweka makazi ya muda katika shule ya sekondari ya Katesh iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Chochote tutakachokipata tutakigawa kwa walengwa kwa sababu hili zoezi ni sehemu ya majukumu yetu na tutalitekeleza kwa uaminifu mkubwa.
“Atakayefanya ubadhilifu wa aina yoyote, serikali haitakuwa na uvumilivu naye, tutachukua hatua,” alibainisha Waziri
Serikali ipo pamoja na nyie, tunajua maswahibu mliyoyapata: wengi wenu mlishapiga hatua za kimaisha, lakini janga hili limeturudisha nyuma,
kikubwa tuwe na moyo wa subira kwa mwenyezi Mungu kwa kuendelea kutulinda.
“Kazi kubwa ilikuwa ilikuwa ya kukabiliana na janga lilipotokea na hatua ya pili ni kurudisha huduma za kijamii na miundo mbinu ya mawasiliano, katika hali ya kawaida,” alifafanua.
katika hatua nyingine waziri Mhagama ameishukuru shirika la umeme TANESCO kwa kurudishia transfoma 76 zilizokuwa zimeharibika na nguzo zaidi ya 60 na hivyo kusaidia kijiji cha Gendabi kilichoathirika na Maporomoko.
“Niwaombe sasa muanze kufanya ufuatilaiji wa nyumba zote zilizokuwa zinapata nishati ya umeme ili wananchi wandelee kupata huduma hiyo alisema,” Waziri.
Awali Luteni Kanali Selestine Masalamadu Mkurugenzi Msaidizi idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, amesema kila familia itapata magodoro 3; masufuria 5, sabuni za miche pamoja na sabuni za unga na nguo za watoto.
Kwa upande wa Bi, Betha Mmari Mwananchi aliyepata adha ya mafuriko ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa Mama Samia kwa Kujali.
“Tunaomba muendele kutuhudumia katika kipindi hiki kigumu kwetu na msituache” alisema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here