Home LOCAL TASAF NJOMBE YATUMIA BILIONI 29 KATIKA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI

TASAF NJOMBE YATUMIA BILIONI 29 KATIKA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI

Mtaalam wa Mawasiliano kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Bi. Zuhura Mdungi akifafanua baadhi ya mambo katika kikaokazi kati ya Mfuko huo na wahariri wa vyombo vya habari waliokatika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi ya TASAF Mjombe.

 Mchumi wa Mkoa wa Njombe na Mratibu wa TASAF Bw. Mussa Selemani akizungumza katika katika kikaokazi kati ya Mfuko huo na wahariri wa vyombo vya habari waliokatika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi ya TASAF Mjombe.

Celina Willson Mhariri kutoka magazeti ya Chama cha Mapinduzi Uhuru na Mzalendo na Mwenyekiti wa Wahariri katika ziara ya kukagua miradi ya TASAF mkoani Njombe akizungumza kwenye kikaokazi hicho kilichofanyika ukumbi wa PSSSF mjini Njombe leo Jumanne Disemba 19, 2023.

……………………… 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Mkoa wa Njombe imesajili kaya maskini 25,855 pamoja kutumia shilingi Bilioni 29 katika kipindi cha mwezi Julai na June mwaka huu kwa ajili ya kusaidia kaya maskini kupata mahitaji muhimu ikiwemo chakula na malezi.

Akizungumza katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari katika ziara ya kutembelea miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Mkoani Njombe kilichofanyika leo Desemba 19, 2023 katika ukumbi wa PSSSF mjini Mjombe , Mchumi wa Mkoa wa Njombe na Mratibu wa TASAF Bw. Mussa Selemani, amesema kuwa kaya za wanufaika wa TASAF zinapungua kadri siku zinavyozidi kwenda.

Bw. Selemani amesema kuwa kupungua kwa kaya maskini kunatokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi kukosa sifa, kuhama bila taarifa pamoja na kujitoa kwa hiari.

Amesema kuwa mpaka sasa zimepungua kaya 709 na hadi kufikia Desemba mwaka huu zimebaki kaya maskini 24, 876.

“Utekelezaji wa mradi wa TASAF Mkoa wa Njombe umegawanyika katika sehemu nne ikiwemo kutoa fedha kwa kaya maskini, kutekeleza  mradi wa kupunguza umaskini, uwezeshaji wa mafunzo kwa vijana wanaotoka katika kaya za wanufaika” amesema Bw. Selemani.

Bw. Selemani amesema kuwa pia wanatekeleza mradi maalamu wa kilimo cha parachichi.

Ameeleza kuwa utoaji wa fedha kwa kaya maskini awamu ya tatu ulianza mwaka 2015 na unafanyika kila baada ya miezi miwili kupitia dirisha la malipo.

Bw. Selemani amesema kuwa malipo ya kaya huusimamiwa na kamati za ulinzi wa jamii ambazo zinaundwa na vijiji pamoja na mitaa kwa lengo la kusimamia utekelezaji.

Amesema kuwa katika kipindi cha kwanza cha madirisha 23 ya malipo wametumia shilingi bilioni 15.19, huku awamu ya pili wametumia bilioni 13.8.

“Kila mwezi tunatumia shillingi bilioni 29 ni sawa na wastani wa shilingi 14,000 kwa kila kaya” amesema Bw. Selemani.

Amesema kuwa mradi wa TASAF umesaidia kuboresha miundombinu muhimu katika sekta ya afya, elimu katika utekelezaji.

Bw. Selemani amesema kuwa halmashauri zimetekeleza jumla ya miradi 384 ya kupunguza umaskini ambayo zimegharimu jumla ya bilioni 25.6.

Amesema kuwa miradi ya kuboresha miundombinu ilikuwa 191 yenye thamani ya bilioni 19.27, huku mradi wa ajira za muda ikiwa 113 ambapo umegharimu bilioni 7.38.

Amebainisha kuwa mradi wa kuongeza kipato ilikuwa 80 ambao walitumia shilingi bilioni 1.895, huku mradi wa elimu ikiwa 67.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here