Home LOCAL THPS NA CDC WAPANUA WIGO HUDUMA JUMUISHI WENYE VVU NA MAGONJWA YASIYO...

THPS NA CDC WAPANUA WIGO HUDUMA JUMUISHI WENYE VVU NA MAGONJWA YASIYO AMBUKIZA

Na: Veronica Mrema

Watu zaidi ya 200,020 wanaoishi na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi {VVU}, wameanza kunufaika na huduma jumuishi ya uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza {NCD’s} kwa kufanyiwa uchunguzi.

Pamoja na hilo, wanapatiwa dawa bila malipo hususan wale wanaogundulika wanakabiliwa na tatizo la Shinikizo la Damu.

Dawa ambayo hivi sasa wameanza kugawiwa bila malipo ni ya kudhibiti Shinikizo la Damu.

Taasisi ya THPS inatekeleza mradi wa Afya Hatua chini ya ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia CDC katika kuwafikia watu hao katika mikoa minne.

Yamebainishwa hayo leo na Mkurugenzi wa Miradi THPS Dkt. Eva Matiko alipozungumza katika mkutano wa masuala ya afya {Tanzania Health Summit}, Dar es Salaam.

“THPS ina malengo ya kuhakikisha huduma jumuishi kwa ajili ya magonjwa yasiyoambukiza inafikia wapokea huduma {wenye VVU} wote,” amesema na kuongeza,

“hivi sasa vituo zaidi ya 245 vinatoa huduma hii, kupima kutambua na kutoa rufaa, kwa mwaka wa fedha 2022/23 baadhi ya mikoa itanufaika na mradi wa CDC.

“Kwa kuweza kutoa dawa kama inavyotolewa kwa dawa za HIV, vile vile dawa za kudhibiti Shinikizo la Damu watakuwa wanapatiwa wateja hawa.

Ameongeza “Hii ni jaribio kuweza kuona kwamba, je hii huduma itawezekana kwa upande wa gharama ili iweze kuendelea na kwenye vituo vingine?

“Lengo kuhakikisha wateja wote wanaohudumiwa na THPS wanapata huduma kamilifu, mpaka sasa hali tunaweza kusema inadhibitika.

“Kwa maana ya kwamba mwanzoni kuanzia januari 2023 idadi ya waliokuwa wanapimwa kikamilifu na kurekodiwa inavyostahili ilikuwa chache.

“Tumeona takwimu zimeonsha mwezi wa tatu ni nusu tu ya wateja waliokuwa wanatembelea walikuwa wana rekodi kamilifu ya shinikizo la damu.

Dkt. Eva amesema hadi kufikia septemba zaidi ya 95% ya wateja waliotembelea vituo walipimwa na kurekodiwa kuhakikisha wanaotembelea wanapata matibabu stahiki.

“THPS Afya Hatua ni mradi unaotekelezwa Mkoani Kigoma, Shinyanga, Pwani na mwaka huu wa tatu umeongezwa Mkoa wa Tanga.

“Tutakuwa tunatekeleza afua kamilifu za HIV katika mikoa hii minne, katika vituo zaidi ya 343 vya kutolea huduma za afya.

“Tunawateja zaidi ya 200020 wanatumia ARVs, 95% wanapimwa na kutambulika kama wana magonjwa yasiyoambukiza hasa Shinikizo la Damu,” amesisitiza.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanufaika wa mradi huo wamesema umekuwa msaada mkubwa kwao.

Nuruhim Omary mwenyeji wa Mwadui Shinyanga Mwadui amesema amegundulika ana maambukizi ya Ukimwi tangu mwaka 2009.

“Nilipata ushauri wa madaktari nikaanzishiwa ARVs, 2021 nilipata tatizo la shinikizo la damu, madaktari walinishauri nikaanza kutumia hizo dawa.

Ameongeza “Sasa nina miaka mitatu natumia hizo dawa, jamii naishauri kupata HIOV si mwisho wa maisha, ukigundulika uanaanza kupata matibabu.

Naye, Juma kigoma 2000 niligundulika nina HIV nilipata ushauri wa madaktari nikaanza ufuasi mzuri wa dawa hadi sasa nina zaidi ya miaka 20.

“2020 niligundulika nina kisukari, kizunguzungu mara kwa mara, nilipopima 31.9 kisukari sasa imefikia 7 nimepima juzi,” amesema.

Ameomba wadau kuweka mazingira rafiki ya sehemu za kutoa ushauri nasaha kwa watu ili wawe na amani pale wanapokuwa wakipatiwa huduma.

Mwakilishi wa CDC Tanzania Dkt. Mahesh Swaminathan amesema pamoja na Shinikizo la Damu pia mradi huo umelenga kutoa afua nyingine dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza ikiwamo chanjo ya HPV kwa wasichana wanaoishi na VVU.

Amesema chanjo hiyo ni muhimu kwani imethibitika kukinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi, pia CDC inawezesha uchunguzi wa awali wa saratani hiyo ili kuwakinga wanawake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here