Home LOCAL RAIS MWINYI AFUNGUA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI CUBA

RAIS MWINYI AFUNGUA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI CUBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesifu ushirikiano unaozidi kuimarika baina ya Tanzania na Cuba, uhusiano huo unatokana na misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Kiongozi wa kwanza wa Mapinduzi ya Cuba Hayati Fidel Castro.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo hii jijini Havana, alipofungua rasmi ubalozi wa Tanzania nchini Cuba. Ubalozi huo uliahirishwa ufunguzi wake tangu mwaka 2019 kutokana na mlipuko wa Uviko-19.

Sherehe hizo zilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Mesa na maafisa wengine wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Steven Byabato pamoja na maafisa wa serikali ya Cuba.

Dk. Mwinyi alibainisha namna Tanzania inavyonufaika kwa ushirikiano na Cuba ukiwemo wa Kitabibu na Elimu pamoja na masuala ya Kilimo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here