Home LOCAL KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA TMDA

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA TMDA

Naibu waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Bw. Adam Fimbo (kushoto), wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, walipotembelea Ofisi za TMDA leo Septemba 11,2023 Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Stanslaus Nyongo, (wa tatu kulia), akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Maabara ya TMDA Dar es Salaam, Catherine Luanda (kulia), wakati wa ziara ya Kamati hiyo walipotembelea Maabara za TMDA Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Stanslaus Nyongo, (katikati), akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Maabara ya TMDA Dar es Salaam, Catherine Luanda (kulia) kuhusu Mashine ya kuchunguza ubora wa Barakoha (Synthetic Blood Penetration tester).

Naibu waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel (kulia) akipokea maelezo kutoka kwa mtaalam wa Maabara na Mchunguzi wa Vifaa Tiba, Saxon Mwambene (wa pili kulia), kuhusu Mashine inayochunguza ubora wa Kondom.

Naibu waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Bw. Adam Fimbo, kuhusu kazi ya kuchunguza ubora wa Bidhaa za tumbaku inayofanywa na Maabara hiyo Jijini Da es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Bw. Adam Fimbo, akifafanua jambo alipokuwa akizungumza katika ziara ya Kamati hiyo, Jijini Dar es Salaam.

Mchunguzi wa Dawa katika Maabara ya TMDA Dar es Salaam, Halima Sembe  akitekeleza majukumu yake

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI imeridhishwa na utendaji wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kwa kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta tija kwa watanzania kwa kuzingatia usalama wa Dawa.

Akizungumza leo Septemba 11, 2023 Jijini Dar es Salaam katika ziara ya Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Ofisi za TMDA, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo, amesema kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada na kazi kubwa katika kuboresha huduma za  Afya nchini,

Mhe. Nyongo amesema kuwa ni jambo rafiki kuwekeza katika sekta ya afya ili kuhakikisha wananchi wanakuwa salama katika matumizi ya dawa na Vifaa Tiba.

“TMDA mnafanya kazi nzuri, kazi yenu inaonekana na tumeridhika, tumekuja kuona na kujifunza” amesema Mhe.Nyongo.

Ametoa wito kwa TMDA kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi kwani watanzania wanawategemea katika usalama wa Afya zao.

Kwa upande wake Naibu waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel, ametoa pongezi kwa TMDA kwa kupiga hatua kubwa katika kusimamia vizuri utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumza alipokuwa akijibu hoja na maswali ya wajumbe wa Kamati hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Bw. Adam Fimbo, amesema kuwa wanaendelea na utekelezaji wa majukumu yao katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuhakikisha Dawa feki hazipati nafasi katika soko.

Aidha, amesema kuwa wanaendelea na jukumu la kusimamia ubora wa Dawa zilizosajiliwa ili kuhakikisha Dawa zote na Vifaa Tiba zinakuwa na ubora kabla ya kufika kwa jamii.

“Ni jukumu letu kulinda afya ya jamii kwa kuhakikisha Dawa na vifaa Tiba zinazokwenda sokoni zinakuwa na ubora” amesema Bw. Fimbo.

Previous articleRAIS DKT. SAMIA : HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA
Next articleUJUMBE WA MADAKTARI WA KICHINA WALIOMALIZA MUDA WA KAZI HAPA NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here