Home BUSINESS BRELA YAENDELEA KUTOA ELIMU NA HUDUMA YA PAPO KWA PAPO GEITA

BRELA YAENDELEA KUTOA ELIMU NA HUDUMA YA PAPO KWA PAPO GEITA

Maafisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), (waliovaa sare), wakiendelea kutoa elimu na huduma ya papo kwa papo kwa Wadau wanaotembelea banda la BRELA katika Maonesho ya Sita (6) ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili Mjini Geita. Maonesho hayo yaliyoanza Septemba 20, 2023, yatahitimishwa Septemba 30, 2023.

Afisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Julieth Kiwelu (kulia), akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kusajili Alama ya Biashara, kwa wajasiriamali wanaoshiriki katika Maonesho ya Sita (6) ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini 2023 Mjini Geita. Maonesho hayo yaliyoanza Septemba 20, 2023 yatahiimishwa Septemba 30, 2023. BRELA inatumia fursa ya maonesho hayo kuwatembelea washiriki mbalimbali katika mabanda ya maonesho hayo na kuwapatia elimu kuhusu umuhimu wa urasimishaji wa biashara.

Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Majina ya Biashara wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA), Bw. Harvey Kombe (kushoto), akimkabidhi cheti cha Usajili wa Jina la Biashara Bw.John Julius Msuya, baada ya kukidhi vigezo vya kusajili Jina la Biashara katika banda la BRELA lililopo katika Maonesho ya Sita (6) ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini 2023 Mjini Geita. Maonesho hayo yaliyoanza Septemba 20, 2023, yatahitimishwa Septemba 30 2023.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here