Home LOCAL MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA KUONDOA BANDAMA

MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA KUONDOA BANDAMA

Hospitali ya Taifa Muhimbili imefanya upasuaji mkubwa wa kuondoa bandama lenye shida kwa mgonjwa kwa njia ya matundu madogo (laparoscopic splenectomy).

Upasuaji huu ni wa kwanza kufanyika hapa nchini ambao umefanywa na madaktari wa upasuaji wa MNH kutokana na ubobezi walionao.

Dkt. Kitembo Salum Kibwana mbobezi wa upasuaji mfumo wa chakula na Ini ndiye aliyeongoza jopo la madaktari, wauguzi na watalaamu wa ganzi na usingizi kufanya Upasuaji huo.

Bandama (wengu) ni kiungo cha mwili chenye nafasi katika mzunguko wa damu. Lipo ndani ya fumbatio ya mwili karibu na mfuko wa chakula ambapo kazi yake kubwa ni kuongeza seli nyeupe za damu na kuondoa seli nyekundu za damu zilizozeeka.

Kwa watoto ina jukumu la kutengeneza seli nyekundu za damu. Watu wazima kwa kawaida wanaweza kuishi bila ya bandama.

Hospitali ya Taifa Muhimbili inaendelea kuboresha huduma zake mbalimbali ikiwemo upasuaji mkubwa, uchunguzi na mifumo ya utoaji huduma kwa ujumla wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here