Home BUSINESS LINDI KUCHELE, MAONYESHO YA MADINI NA FURSA ZA UWEKEZAJI

LINDI KUCHELE, MAONYESHO YA MADINI NA FURSA ZA UWEKEZAJI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Zuwena Omary Jiri akizungumza ofisini kwake juu ya maonyesho ya madini na fursa za uchumi yatakayofanyika Agosti 21 hadi 26 Mjini Ruangwa yenye kauli mbiu ya wekeza Lindi kwa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya jamii

Na: Mwandishi wetu, Lindi

MKOA wa Lindi unatarajia kufanya maonyesho ya madini na fursa za uwekezaji yatakayohusisha wafanyabiashara na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Mkoa wa Lindi yanapatikana na kuchimbwa madini ya aina mbalimbali ikiwemo dhahabu, nickel, ganeti ya kijani, manganese ore, marble, gypsum na ulanga (kinywe).

Katibu Tawala wa mkoa wa Lindi, (RAS) Zuwena Omary Jiri amesema maonyesho hayo yatafanyika kwa muda wa siku sita wilayani Ruangwa Agosti 21 hadi 26.

RAS Zuwena amesema tamasha na maonyesho hayo yatahusisha fursa mbalimbali zinazopatikana mkoani Lindi ikiwemo madini, utalii, kilimo, mifugo na uvuvi.

“Lengo ni kuangazia fursa zilizopo mkoani Lindi na kujenga jukwaa ambalo wadau wa sekta ya madini na sekta shirikishi watapata nafasi ya kujadiliana, kubadilishana uzoefu na kutangaza fursa zilizopo mkoani Lindi,” amesema RAS Zuwena.

Amesema wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wafanyabiashara, wawekezaji na wapenda maendeleo tofauti kutoka ndani na nje ya nchi watashiriki tamasha na maonyesho hayo.

Amesema kauli mbiu ya maonyesho hayo ni wekeza Lindi kwa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here