Home BUSINESS BRELA YATOA ELIMU KWA VIKUNDI VYA KIJAMII MAONESHO YA SABASABA

BRELA YATOA ELIMU KWA VIKUNDI VYA KIJAMII MAONESHO YA SABASABA

Afisa Sheria Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Andrew Malesi (mwenye suti ya Bluu), akitoa elimu ya Miliki Ubunifu eneo la usajili wa alama za Biashara na Huduma, kwa wanachama wa Shirikisho la Vikundi vya kijamii mkoa wa Dar es Salaam (TFUP), waliotembelea Banda la BRELA kupata elimu ya namna wanavyoweza kusajili Biashara zao na kupata Leseni, ili kuongeza ufanisi katika shughuli zao za ujasiriamali. (wa tatu kushoto), ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikali (BRELA), Bi. Roida Andusamile.

BRELA imeweka kambi katika maonesho hayo ambapo kwa mwaka huu wametenga maeneo manne tofauti yatakayowawezesha  wananchi kupata huduma katika mabanda yao kwa wakati, kulingana na mahitaji yao.

Maeneo hayo ni pamoja na Banda la huduma za Miliki Ubunifu, Banda lingine linatoa huduma jumuishi, na mabanda mawili yanatoa huduma za papo kawa hapo.

Msaidizi wa Usajili Kurugenzi ya Makampuni na majina ya Biashara Bi. Maryglory Mmari (kulia), akitoa elimu ya usajili wa majina ya Biashara na makampuni kwa wanachama wa Shirikisho la Vikundi vya kijamii Mkoa wa Dar es Salaam (TFUP) waliofika katika Banda la Brela kupata elimu kwenye maonesho ya Sabasaba JIjini Dar es Salaam. (wa pili kulia), ni ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikali (BRELA), Bi. Roida Andusamile.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here