Home BUSINESS BoT YATOA ELIMU KWA WANANCHI UMUHIMU WA KUWEKA AKIBA

BoT YATOA ELIMU KWA WANANCHI UMUHIMU WA KUWEKA AKIBA

Afisa Sheria Mwandamizi, Kurugenzi ya Huduma Sekta ya Kifedha, Bw.  Ramadhani Myonga (kushoto), akiwa na Bw. Lucas Maganzi, Huduma za Kurugenzi ya Ujumuishi na Ustawi wa Huduma za Fedha (wa pili kushoto), wakitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la BoT kwenye Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Na: Hughes Dugilo, Dar es Salaam.

Benki Kuu ya Tanzania (BOT), imewashauri watanzania kuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba itakayowaezesha kufikia malengo yao katika kukabiliana na changamoto za kimaisha.

Hayo yamezungumzwa na Afisa Sheria Mwandamizi, Kurugenzi ya Huduma Sekta ya Kifedha, Ramadhani Myonga, amesema BoT katika mahojiano maalum kwenye maonesho ya 47 ya Biashara ya Kamataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Juliaus Nyerere Jijini Dar es Salaam,.

Amesema BoT ina jukumu la kuuelemisha umma kuhusu umuhimu wa kuweka akiba, na kwamba watu wengi wamekosa elimu hiyo ya uwekezaji wa akiba, hivyo wapo kwenye maonesho hayo ili kutoa elimu ya  fedha kwa wananchi.

Ameongeza kiwa wanatoa elimu hiyo kwa mwananchi mmoja mmoja, Vikundi na Taasisi mbalimbali ili kuwasaidia kutambua umuhimu wa kujiwekea akiba itakayowawezesha kukabiliana na changamoto za maisha.

“Tunawafundisha namna ya kutengeneza Bajeti, kutengeneza vipaumbele, kujua namna ya kuwekeza, lakini pia kujifunza namna nzuri ya kuweza kulipa Kodi pamoja na mpangilio mzuri wa matumizi ya fedha, kujua kati ya matumizi na mapato unaweza vipi kuwa na usawa, ili mwisho wa siku uweze kuwa na kipato cha kuzalishia, kitakachopelekea kuwa na akiba.

“Vile vile tunatoa elimu ya akiba, kwa kuwaeleza akiba ni nini, faida zake na inawekezwa wapi”  amesema Myonga.

Aidha ameongeza kuwa wanatoa elimu kwa watoto kuwajengea uwezo na kujifunza namna ya kuwekeza fedha kuanzia wakiwa na umri mdogo, ili wakiwa na umri mkubwa wawe na uelewa wa masuala mbalimbali ya kifedha, na nidhamu ya fedha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here