Home BUSINESS NI MAKOSA KUJIHUSISHA NA BIASHARA NDOGO ZA HUDUMA ZA FEDHA BILA LESENI...

NI MAKOSA KUJIHUSISHA NA BIASHARA NDOGO ZA HUDUMA ZA FEDHA BILA LESENI YA BENKI KUU

Benki Kuu ya Tanzania imebaini kuwa kuna baadhi ya taasisi, kampuni na watu binafsi wanaojihusisha  na biashara ya kutoa mikopo bila ya kuwa na leseni, jambo ambalo ni kinyume na Kifungu cha 16(1) cha  Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018. Aidha, taasisi, kampuni na mtu binafsi wasio na  leseni hawaruhusiwi kufanya biashara ya kukopesha. Kufuatia kifungu cha 16(2)(a) cha Sheria ya  Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, hatua zitakazochukuliwa kwa ukiukaji wa Sheria hiyo ni  pamoja na faini isiyopungua Shilingi Milioni 20 au kifungo cha muda usiopungua miaka miwili.  

Benki Kuu ya Tanzania inawakumbusha watoa huduma ndogo za fedha waliokwisha kupata leseni  kufuata sheria, kanuni na miongozo inayotolewa na Benki Kuu ya Tanzania ikiwemo kuwapa wakopaji  mikataba, kuonyesha riba ya mkopo kama ilivyopitishwa kwenye sera ya mkopo, gharama nyingine zote  wanazotoza, na riba kukokotolewa kwa mwezi na sio kwa siku. 

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuwaasa wananchi kuepuka kukopa au kufanya biashara na taasisi,  kampuni au mtu binafsi ambao hawana leseni. Aidha, orodha ya taasisi, kampuni na watu binafsi wenye  leseni za biashara ya kukopesha zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania inapatikana kwenye tovuti ya  Benki Kuu ambayo ni www.bot.go.tz na kwenye matawi yake yote.  

Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na:  

Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha Idara ya Usimamizi wa Taasisi za Huduma Ndogo za  Fedha Benki Kuu ya Tanzania, 2 Mtaa wa Mirambo, S.L.P 2939 Dar es Salaam Simu Na. +255-22-223- 5585; Barua Pepe: info@bot.go.tz or botcommunications@bot.go.tz  

GAVANA 

BENKI KUU YA TANZANIA 

Previous articleKINANA AKUTANA NA BALOZI WA BRAZIL NCHINI TANZANIA
Next articleDAWASA YAANZA RASMI ZOEZI LA UTOAJI VIBALI MAGALI YA KUZAMBAZA MAJISAFI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here