Home BUSINESS Dkt. ABDALLAH: SERIKALI ITAENDELEA KUWAENZI, KUWALINDA NA KUWATUNZA WAWEKEZAJI NCHINI

Dkt. ABDALLAH: SERIKALI ITAENDELEA KUWAENZI, KUWALINDA NA KUWATUNZA WAWEKEZAJI NCHINI

Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa pamoja na uongozi wa Mkoa wa Iringa akiangalia marine board zinazotengenezwa na malighafi za vinia alipotembelea Kiwanda cha East Africa Shenyuan Group kilichopo Mufindi Iringa Juni 24, 2023 baada ya kusikiliza changamoto za Wamiliki wa Viwanda hivyo. Kiwanda hicho kinachozalisha Plywood, Marine Boards na MDF kwa kutumia malighafi ya vinia inayotokana na Miti.

Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa pamoja na uongozi wa Mkoa wa Iringa na wakitembelea Kiwanda cha Yisen International Company kilichopo Mufindi Iringa Juni 24, 2023 baada ya kusikiliza changamoto za Wamiliki wa Viwanda hivyo. Kiwanda hicho kinachozalisha Plywood, Marine Boards na MDF kwa kutumia malighafi ya vinia inayotokana na Miti.

 Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa pamoja na uongozi wa Mkoa wa Iringa wakiangalia kipande cha vinia aliptembelea Kiwanda cha Cheda Mas Wood kilichopo Mufindi Iringa Juni 24, 2023 baada ya kusikiliza changamoto za Wamiliki wa Viwanda hivyo. Kiwanda hicho kinachozalisha malighafi ya vinia inayotokana na Miti na kuviuzia viwanda vingine kutengeneza bidhaa za mwisho.

Wafanyakazi wa Kiwanda cha Yisen International Company kilichopo Mufindi Iringa wakiendelea na kazi ya uchakataji wa vinia inayotumika kutengeneza plywood, marine boards, samani, vifaa vya michezo, makasha ya kusafirisha bidhaa na ujenzi wa majengo na miundombinu mbalimbali.

Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwaenzi, kuwalinda na kuwatunza wawekezaji wanowekeza nchini.

Aidha, ametoa rai kwa Wawekezaji kuendelea kuwekeza kwa kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira bora na wezeshi pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini (MKUMBI)

Dkt. Abdallah ameyasema hayo kwa Juni 24,2023 Mkoani Iringa Wilaya ya Mufindi alipokutana na kusikiliza changamoto za Wamiliki wa Viwanda vya kuzalisha bidhaa za mazao ya misitu hususani Vinia inayotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali kama plywood MDF, na marine boards.

Akisikiliza changamoto zao baada ya kutembelea baadhi ya Viwanda vikubwa vinavyozalisha Vinia mpaka zao la mwisho na vidogo vinavyozalisha vinia peke yake, Dkt. Abdallah amesema Wizara kwa itashirikiana na Mkoa wa Iringa pamoja na Wakala wa Misitu (TFS ) kutatua changamoto zote zilizojitokeza ili wawekezaji hao waendelee kuzalisha bidhaa hizo kwa tija

Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bi. Asifiwe Mwakibete ametoa kwa wawekezaji kuendelea kuwekeza katika viwanda vya mazao ya misitu mkoani humo kwa kuwa malighafi ya miti inapatikana kwa wingi na wananchi waendelee kupanda miti kwa kuwa soko la miti ya mbao ni kubwa Mkoani humo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Bw., Ayoub Kambi amesema kwa kushirikiana na Mkoa wa Iringa wataweka mikakati ya kutatua changamoto zote zilizojitokeza kwa wawekezaji wa viwanda vinavyotengeneza bidhaa kwa kutumia Vinia

Vinia ni moja ya mazao ya misitu yanayohandisiwa ( Engeneered Wood Products(EWP) inayotumika kutengeneza moja kwa moja bidhaa za mazao ya mbao. Vilevile hutumika kutengeneza plywood, marine boards, samani, vifaa vya michezo, makasha ya kusafirisha bidhaa na ujenzi wa majengo na miundombinu mbalimbali.

Wilaya ya Mufindi ina viwanda 27 vinavyoshughulika na uzalishaji wa vinia. Kati ya hivyo viwanda 6 vinauwezo wa kuzalisha bidhaa hadi hatua ya mwisho kama plywood MDF na marine board kwa kutumia vinia na viwanda vingine vinaishia hatua ya malighafi ya vinia.

Previous articleMAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 25 – 2023
Next articleCHONGOLO AKEMEA TABIA YA WIZI WA VIFAA VYA UJENZI MRADI WA RING ROAD DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here