Home LOCAL DAWASA YAANZA RASMI ZOEZI LA UTOAJI VIBALI MAGALI YA KUZAMBAZA MAJISAFI

DAWASA YAANZA RASMI ZOEZI LA UTOAJI VIBALI MAGALI YA KUZAMBAZA MAJISAFI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeanza rasmi zoezi la usajili na utoaji wa vibali kwa magari ya kusambaza majisafi (water bowsers) kwa mwaka 2023/2024 linalofanyika katika eneo la Tegeta Wazo, Kibamba, Mbezi spencon, Kimara suka, Mapinga, Kibaha na Chalinze.

Lengo la zoezi hili ni kuratibu huduma ya Majisafi kupitia magari na kuhakikisha huduma inayotolewa kwa wananchi ambao hawajafikiwa na miundombinu ya DAWASA inakidhi vigezo vilivyowekwa na Mamlaka.

Zoezi hili lilianza tarehe 19 hadi 30 Juni 2023 na malipo ya usajili yatafanyika kupitia mfumo wa Serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here